Picha hii ya mvulana anayeonekana
kujiuliza maswali si haba akilini mwake akiwa na Mzungu imesambazwa mara
nyingi sana mtandaoni.Wengi wamekuwa wakiitumia kukejeli vyombo
vya habari, mataifa na mashirika ya kutoa misaada kutoka Magharibi kwa
mtazamo wao kuhusu Afrika. Kunao wanaoitumia hata hivyo kuuliza maswali
ya kijumla tu.
Lakini je, wajua picha hii ilitoka wapi? Mvulana huyu ni nani?
Picha
hii ilianza kuenea sana mtandaoni baada ya kupakiwa kwenye tovuti ya
Reddit miaka mitatu iliyopita na mwanamume kutok Texas, Marekani
aliyevutiwa nayo baada ya kuiona kwenye ukurasa wa Facebook wa rafiki
yake.
Mwanamke aliye kwenye picha hiyo ni Heena Pranav, daktari mwenye umri wa miaka 28 anayeishi Chicago.
Mwaka
2012, alipokuwa mwanafunzi, alizuru mji wa Gulu, kaskazini mwa Uganda
kusaidia kwenye mradi wa kuwasaidia wanawake walioathiriwa na vita vya
wapiganaji wa Lords Resistance Army. Mradi huo ulisimamiwa na shirika
laPros for Africa, linaloongozwa na mtawa Mkatoliki, Rosemary Nyirumbe.
Picha
hiyo haikuhusiana na mradi huo na Pranav, akizungumza na BBC Trending
radio, amesema alikutana na mvulana huyo sokoni na anakadiria alikuwa na
umri wa miaka miwili au mitatu.
"Nilikuwa na wanafunzi wengine
wakati huo, na tulikuwa tunapiga gumzo na nikaona mvulana mdogo,
aliyenivutia sana,” Pranav alisema.
“Mamake alikuwa karibu akifanya kazi sokoni. Nilimwendea mvulana huyo kumsalimia na kucheza naye … alikuwa mchangamfu sana."
Mvulana
huyo hakuzungumza Kiingereza, na Pranav naye haelewi lugha za wenyeji.
Lakini mkutano wao mfupi ulinakiliwa kwenye picha iliyopigwa na mmoja wa
wanafunzi kwenye kundi la Pranav. Binti huyo anasema hakuwa amewahi
kusikitia Reddit hadi pale rafiki yake alipoipakia picha hiyo huko na
ikasambaa sana.
"Sikudhani hili lingelitokea,” anasema.
“Kungelikuwa na uwezekano ningetaka sana mtoto huyu na mamake wajue
kuhusu haya na wanufaike kiasi kutokana nayo, kwa sababu nadhani
alitumiwa bila kupata manufaa yoyote.”BBC Trending inamtafuta
mtoto huyu, kwa hivyo iwapo unamfahamu au unajua familia yake, tutumia
barua pepe kupitia trending@bbc.co.uk.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni