Breaking News

Jumatano, 4 Novemba 2015

TB Joshua atua Tanzania

Mhubiri mashuhuri kutoka Nigeria TB Joshua ni miongoni mwa wageni mashuhuri watakaohudhuria sherehe ya kumuapisha John Pombe Magufuli kuwa rais mpya wa Tanzania Alhamisi.
Bw Joshua ambaye ni mhubiri wa kanisa la Church of All Nations aliwasili jijini Dar es Salaam Jumanne. Baada ya kuwasili kwa mhubiri huyo, Bw Magufuli aliandika kwenye Twitter: "Tumshukuru Mungu, tumepata ugeni wa Nabii TB Joshua, atashiriki nasi katika sherehe nitakapoapishwa kuwa Rais wa awamu ya Tano wa Tanzania."
                                          TB Joshua alimtembelea Rais Kikwete ikuluni Dar es Salaam 
Baadaye, alikutana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika ikulu ya Dar es Salaam. Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, ambaye ni rafiki wa karibu wa Bw Magufuli, pia anatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo.
Tayari muungano wa Cord unaoongozwa na Bw Odinga umeahirisha shughuli ya kuwasilisha sahihi za kuunga mkono marekebisho ya katiba kwa Tume ya Uchaguzi ya Kenya (IEBC) ili kuhudhuria sherehe hiyo. Muungano huo ulikuwa awali umepanga kuwasilisha sahihi hizo leo.
Bw Magufuli, aliyekuwa mgombea wa chama tawala cha CCM ataapishwa kuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada yake kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Novemba 25, matokeo ambayo yalipingwa na chama kikuu cha upinzani nchini humo Chadema.
Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Chadema Edward Lowaasa aliibuka wa pili, kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania. Chanzo BBC Swahili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni