Kauli mbiu ya Hapa Kazi tu imeanza kutumika rasmi jana ikiwa ni saa tatu baada ya kuingia Ikulu kufuatia uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Mcheche Masaju.
Jaji Masaju akiapishwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
Uteuzi huo umefanyika wakati ndugu jamaa na marafiki wa Rais wa awamu ya tano katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Joseph Magufuli , wakiungana na watanzania pamoja wakuu wa nchi nane Barani Afrika, pamoja na wawakilishi wa nchi 40 waliofika Tanzania kushuhudia tukio la kihistoria la kuapishwa kwa Rais huyo katika Uwanja Uhuru jijini Dar es Salaam baadaye kuungana na wageeni wake kupata chakula cha mchana katika bustani ya Ikulu ya Dar es Salaam.
Mbali na uteuzi huo pia Rais Dk Magufuli tayari ameitisha kikao cha kwanza cha bunge la 11 la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, November 17 huku uteuzi wa Waziri Mkuu ukifatarajia kufayika November 19 mwaka 2015.
Jaji Frederick Mwita Werema, akizungumza na wanahabari.
Jaji Masaju aliteuliwa January mwaka huu kushika nafasi hiyo katika serikali ya awamu ya nne ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.
Uteuzi wa Masaju ulianza Ijumaa ya, Januari 2, 2015 na kuapishwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.Kabla ya uteuzi wake,Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jaji Masaju aliteuliwa na Kikwete kushika nafasi ya aliyekuwa Mwanasheria mkuu wa Serikali yake Jaji Frederick Mwita Werema, aliyefukuzwa kazi kwa kashfa ya wizi wa fedha za Escow.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni