Breaking News

Jumamosi, 7 Novemba 2015

Hii ndiyo hekma ya viongozi Tanzania

TANZANIA nikati ya nchi chache duniani, na ya kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwa ushawishi na kupatanisha mahasimu mbalimbali.

Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius kambarage Nyerere, alikuwa mpatanishi mkubwa duania hususan Bara la Afrika, mpaka mauti yanamkuta alikuwa mpatanishi na mlezi wa Serikali ya Burundi,Rwanda na DR Congo.


Rais Dk Magufuli (katikati), baada ya kuwapatanisha mahasimu katika siasa za Kenya, (kulia) Raila Odinga na mkewe, kushoto Rais Uhuru Kenyatta.

Rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa pamoja na Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete, waliendeleza hekma hiyo katika nchi mbalimbali ikiwemo Kenya, baada ya kufanikiwa kuwapatanisha mahasimu wawili wa nchi hiyo Rais wa awamu ya tatu Mwai Kibaki na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga.

Kushoto Mke wa Rais Kenyatta, wapili kushoto mke wa Rais Dk magufuli

Ikiwa ni saa sita baada ya kuapishwa Rais mpya wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungo wa Tanzania Dk John Pombe Joseph Magufuli, aliweza kuwapatanisha mahasimu wa Serikali ya Kenya Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa ODM ambacho ndicho chama kikuu cha upinzani Raila Odinga,katika Ukilu ya Dar es Salaam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni