Huyu ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali ambaye pia aliwahi kuwa
Mjumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge la Katiba na Mshauri wa Mwenyekiti
wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba.
Kuna baadhi ya watu wameshangaa kusikia akipitishwa na Kamati Kuu ya CCM
kama mmoja wa wanaCCM watatu watakaopigiwa kura na wabunge wa CCM. Ni
watu wachache watakuwa waliamini kama anaweza kupitishwa kwenye tatu
bora hasa walipolinganisha na majina ya wanaCCM wengine waliochukua
fomu.
Kile alichokifanya Dk. Tulia mpaka kufika kwenye tatu bora hakina
tofauti na kile alikifanya Dk. Magufuli mpaka kufika kwenye tatu bora ya
CCM katika tiketi ya Urais wa Tanzania.
Kuna uwezekano mkubwa kuna mikono ya ''kitengo'' cha CCM/Serikali katika safari ya Dk. Tulia Ackson kama ilivyokuwa katika safari ya Rais Magufuli. Watu wa ''kitengo''
kwa sasa wanataka kuhakikisha hakuna makundi ambayo ni chanzo cha
kukidhoofisha chama na serikali kama ilivyokuwa katika utawala wa Rais
Kikwete.
Ameenda kimya kimya kuchukua fomu za kugombea Uspika kama alivyofanya Dk. Magufuli wakati akichukua fomu za Urais.
Dk. Tulia alikataa kuongea na waandishi wa habari kabla na baada ya
kuchukua fomu pamoja na waandishi wa habari kusisitiza aongee nao hata
machache baada ya kuchukua fomu. Hata Dk. Magufuli alikataa kuongea na
waandishi wa habari kabla na baada ya kuchukua fomu ya Urais.
Hana makundi ndani ya CCM ukilinganisha na wagombea wengine kama alivyokuwa Rais Magufuli wakati wa mchakato wa Urais.
Dk. Tulia alionekana kuwa cool, calm, and collected katika zoezi zima la
mchakato wa kumpata Spika pamoja na kuwa ''CCM outsider'' ukilinganisha
na wanaCCM wengine waliochukua fomu.
Kwa tell-tale signs kama hizi siwezi kushangaa kusikia amekuwa Spika wa Bunge la Tanzania.
Wahenga walisema Simba mwenda kimya(pole) ndiye mla nyama!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni