Breaking News

Jumapili, 8 Novemba 2015

Ukawa kususia hotuba ya Rais Magufuli Bungeni


WAKATI vyama vya upinzani wenye muungano wa Umoja wa Katiba ya Watanzania (Ukawa) vikiendelea kukana kwamba hawautambui ushindi wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Joseph Magufuli.

Picha hii inaonyesha matamshi mbalimbali ya viongozi wa Chadema juu ya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kabla ya kujiunga na chama hicho.

Taarifa za ndani ya umoja huo unasema kwamba wamepanga kutoka nje ya Bunge kama walivyofanya mwaka 2010, wakati walipopinga ushindi wa aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete.

Taarifa hiyo inadai kwamba wabunge wote wa Ukawa watatoka nje ya Bunge wakati Rais Dk Magufuli atakapokuwa akihutubia bunge hilo.Tayari Rais ameshamteuwa Jaji George Mcheche Masaju kuwa mwanasheria Mkuu wa Serikali yake na kuitisha kikao cha kwanza la Bunge la 11 kuwa November 17 mwaka huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni