1.12pm:Sasa rais Magufuli akiandamana na mkewe wanaondoka katika uwanja wa Uhuru baada ya kuapishwa rasmi.
1.09pm:Amewataka
viongozi wa upinzani kushirikiana na serikali yake akisisitiza kuwa
uchaguzi umekwisha na kwamba rais aliyechaguliwa ni John Pombe Magufuli
1.06pm:Magufulu aipongeza tume ya
uchaguzi kwa kufanya uchaguzi ulio huru mbali na vyombo vya usalama
vilivyoimarisha amani.Awashukuru wanahabari kwa kuwaelimisha raia wa
Tanzania
1.05pm:'Sasa ni kazi tu' awataka viongozi wa upinzani kushirikiana kwa lengo la kuendeleza na kuwahudumia watanzania
1.04pm:''Nashukuru wagombea wanzangu kwa kutupa chanagmoto,tumejifunza mengi kutoka kwao''.
1.03pm:''Natambua
kwamba nina jukumu kubwa la kuwafanyia kazi watanzania,lakini hatahivyo
tumuweke mungu mbele ili kutekeleza ahadi hizo.
1.02pm:Magufuli:Nawashkuru watanzania kwa kunichagua kwa kura nyingi ili kuongoza taifa kwa miaka mitano ijayo.
1.01apm:Magufuli:Nawashukuru viongozi mbali,mbali waliowasili hapa ili kujumuika nami katika sherehe hii muhimu.
1.00pm:Namshkuru sana mwenyezi mungu aliyetujalia kuwepo hapa pamoja na viongozi wa dini.
12.58pm:Na sasa ni wakati wa rais John Pombe Magufuli kulihutubia taifa.
12.06am:Marais na viongozi mbalimbali waliowasili katika hafla hiyo watambulishwa kwa wananchi waliojaa katika uwanja huo.
12.00am:Na sasa kamanda wa jeshi anaomba rukhsa ya kuondoka uwanjani.
11.56am:Ndege za kijeshi zinapita juu ya uwanja wa Uhuru kutoa heshima kwa rais mpya wa taifa hilo John Pombe Magufuli.
11.27am:Rais Magufuli alikagua gwaride la heshima
11.23am:Mizinga 21 ya kumkaribisha rais mpya wa Tanzania John Pombe Magufuli yapigwa
11.22am:Jeshi laomba rukhsa kutoka kwa rais mpya wa Taifa la Tanzania John Pombe Magufuli
11.20am:Jakaya Mrisho Kikwete sasa awasalimia viongozi waliofika katika jukwaa la waheshimiwa wakiwemo marais mbalimbali.
11.18am:Sasa jeshi lamuaga aliyekuwa rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete na aliyekuwa makamu wake Gharib Bilal
10.55am:Makamu wa rais wa Kwanza mwanamke nchini Tanzania Samia Suluhu Hassan aapishwa
10.51am:Rais mpya wa Tanzania apewa mkuki na ngao ya ishara ya kuchukua madaraka.
10.48am:''Mimi
John Pombe Magufuli naapa nitatenda kazi zangu za urais kwa mujibu wa
sheria na mila na desturi za muungano wa Tanzania,ewe mwenyezi mungu
nisaidie''
10.47am:Rais mteule John Pombe Magufuli aapisshwa .Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pia amewasili hapa.
10.45am:Na sasa aliyekuwa rais wa
taifa hilo Jakaya Kikwete amekuwa raia wa kawaida baada ya bendera ya
utawala wake kushushwa hapa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
10.40am:Wimbo wa Taifa la Tanzania wapigwa na baadaye bendera ya rais Kikwete itashushwa ili kuashiria mwisho wa uoingozi wake.
Mizinga 21 ya kutoa heshima za mwisho kwa rais Jakaya Kikwete yapigwa.
10.21am:Gari la gwaride la kijeshi
lililombeba rais Kikwete sasa lauzunguka uwanja huo huku wananchi
waliojjaawa na furaha wakimsalimia kwa kumpungia mkono.
10.20am:Na
sasa msafara wa Rais Jakaya Kikwete wawasili katika uwanja wa Uhuru
.KIkwete baadaye anaonekana kuingia katika gari rasmi la gwaride katika
uwanja wa uhuru na kuwapungia mkono maelfu ya wananchi waliojaa katika
uwanja huo.
10.15am:Rais Mteule John Pombe Magufuli awasili katika sherehe hizo na kulakiwa na jaji mkuu Othman Chande.
9.48am:Rais wa Rwanda Paul Kagame
anawasili katika uwanja wa uhuru na kuketi bega kwa bega na waliokuwa
marais wa taifa hilo Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.
9.47am:Rais
wa kisiwa cha Zanzibar Dokta Ali Mohammed Shein amewasili katika uwanja
wa Uhuru na anaonekana hapa akisalimiana na rais mstaafu wa Tanzania
Hassan Mwinyi.Kumbuka kiongozi huyo wa Zanzibar aliongezewa mda wa
kuhudumu katika kisiwa hicho baada ya tume ya uchaguzi kufutilia mbali
matokeo ya uchaguzi wa urais katika kisiwa hicho.
9.43am:Rais mteule John Pombe Magufuli atakuwa rais wa awamu ya tano kuchaguliwa nchini Tanzania tangu taifa hilo lijipatie Uhuru.
9.39am:Vilevile aliyekuwa waziri
mkuu nchini Kenya Raila Odinga ambaye ni rafiki mkubwa wa rais mteule
John Pombe Magufuli,rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph
kabila pamoja na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ni baadhi ya viongozi
waliowasiliili kuhudhuria sherehe hiyo ya kihistoria.
9.35am:Miongoni
mwa viongozi wanaotarajiwa katika hafla hii ni pamoja na rais wa Kenya
Uhuru Kenyatta ambaye tayari ameondoka katika uwanja wa Jomo Kenyatta
Jijini Nairobi akiandamana na Mkewe bi. Margeret Kenyatta na anatarajiwa
kuwasili katika uwanja wa sherehe hizi wakati wowote kutoka sasa
9.30am:Gwaride
la kijeshi tayari limejiandaa vilivyo ikiwemo wanajeshi waliovalia sare
za rangi tofauti hapa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
8:00 am Mataifa mbalimbali yamekuwa yakituma risala za pongezi kwa Tanzania na kwa Rais Mteule John Magufuli.
Wa kwanza kutuma risala za pongezi walikuwa ni:
Rais wa Rwanda Paul Kagame na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Saharawi Mohammed Abdelaziz.
Katika
salamu zake kwa Rais Mteule Magufuli, Bw Kagame amesema: "Kufuatia
kuchaguliwa kwako kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, napenda
kukutumia Mheshimiwa salamu za dhati, pongezi na heri nyingi kwa niaba
yangu mwenyewe, Serikali yangu na wananchi wa Rwanda.”
Naye Rais
Abdelaziz amemwambia Rais Mteule Magufuli: “Sisi tuna uhakika kuwa chini
ya uongozi wako wa busara, Tanzania itaendelea kusonga mbele na kupata
maendeleo na ustawi mkubwa zaidi.”
7:10 am
Viongozi wa baadhi ya mataifa ya Afrika wanatarajiwa kuhudhuria wakiwemo
Jacob Zuma kutoka Afrika Kusini, Robert Mugabe kutoka Zimbabwe na
Filipe Nyusi wa Msumbiji. Mhubiri mashuhuri kutoka Tanzania TB Joshua
pia atahudhuria sherehe hiyo.
7:00 am Watumbuizaji wanaotarajiwa kutumbuiza wakati wa sherehe walifika uwanjani mapema na ala zao.
6:45 am Uwanja umeanza kujaa watu.
Wengi wa waliofika mapema wanafurahisha kujipiga, kupigana na kupigwa
pichwa kuweka kama kumbukumbu za siku hii.
6:30 am Uwanja wa Uhuru umepambwa ukapambika
6:30 am Waandishi wa BBC wamo katika uwanja huo kukuletea habari kadiri zinavyochipuka.
6:30 am Sherehe ya kumuapisha Bw Magufuli inafanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
6:00 am. HABARI YA ASUBUHI?
Rais
Mteule wa Tanzania John Pombe Magufuli anaapishwa leo kuwa rais wa
awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kutangazwa
mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 25.
Rais Magufuli alipata asilimia 58.46 ya kura zilizopigwa kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania. chanzo BBC/Swahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni