Breaking News

Jumatatu, 16 Novemba 2015

Moni ya mdau:Afrika kulilia Paris ni Upumbavu



Afrika Kulilia Ufaransa :Kama si unafiki ni nini? Kafiwa jirani chozi mpaka kifuani! Sijafurahia na ninalaani Mauaji ya watu wasio na hatia Ufaransa na popote Duniani, nawapa pole wafiwa na nawaambia Wafaransa mjifunze kwa hilo na mjifunze UTU.  Na nachukuwa nafasi hii kuwaambia Waafrika wenzangu Tukome kujipendekeza!
Unajua kwamba, Wafaransa wamewakalia na kuua mamilioni ya waafrika, waliiba na kuharibu mali, Ardhi na kuua wanyama.
Katika vita ya Uhuru wafaransa waliwaua wa Algeria zaidi ya Milioni moja, Dunia haiumii wala haizungumzii hilo.
Watu wa dunia ya leo wakiwepo baadhi ya waafrika wenzetu wameshikwa na uchungu sana, wanatuma ujumbe kuwa Mwafrika si Binadamu mwenye thamani sawa na wafaransa waliouawa.
Dunia inajua kuwa wafaransa hawa wanashirikiana na Marekani kupiga mabomu Afrika ya kaskazini na Mashariki ya kati, kuvamia na kuua nchini Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Lakini Dunia haisikii uchungu.
Wafaransa hawa walipokuwa wanaondoka kuziacha nchi za Afrika walichukua mali zao zote na kuharibu kila kitu ambacho walikiweka; Shule, majengo, walichoma magari, vitabu, dawa, tafiti. Waliangamiza wanyama kama farasi, ng'ombe na kuharibu mashamba na chakula cha kwenye maghala kwa sumu na moto. Pamoja na roho mbaya hii yote nchi 14 za Afrika zilizotawaliwa na Mbwa hawa bado zinaendelea kulipa kodi ya UKOLONI kwa Ufaransa tangu uhuru wao mpaka leo!
'Ashakum si matusi'
Mbona siwaoni waafrika wenzangu kushtuka na kulaani haya, hawa mabwana Magharibi wametuloga na uchwai gani? Walianza kuchezea Konzi za Dada zetu, wameshika migongo ya Mama zetu tunawachekea, wamewaua Baba zetu, leo tunaacha kuomboleza misiba yetu waliyotuachia tunawaombolezea wao kwa kwakushusha Suruali zetu nusu mlingoti, tukitiwa Ujiti hadharani tutaficha wapi nyuso zetu?
Na
Maembe Vitali

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni