Breaking News

Jumapili, 3 Januari 2016

Mauaji ya mhubiri Saudi Arabia yazua joto


TehranImage copyrightAFP
Image captionWaandamanaji mjini Tehran waliwasha moto majengo ya ubalozi wa Saudi Arabia
Marekani imeeleza wasiwasi wake kuhusu hali eneo la Mashariki ya Kati baada ya Saudi Arabia kumuua mhubiri mashuhuri wa Kishia Sheikh Nimr al-Nimr.
Marekani imesema mauaji hayo huenda yakazidisha uhasama baina ya madhehebu mbalimbali eneo hilo. Idara ya mashauri ya kigeni ya Marekani imewahimiza viongozi wa eneo hilo kutia juhudi maradufu kupunguza mvutano.
Nchini Iran, waandamanaji waliokasirishwa na mauaji ya mhubiri huyo waliwasha moto majengo ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Tehran.
Aliunga mkono maandamano dhidi ya utawala wa Saudi Arabia katika mkoa wa Mashariki wenye Washia wengi mwaka 2011.
Kupitia taarifa, msemaji wa wizara ya mashauri ya kigeni ya Marekani John Kirby ametoa wito kwa serikali ya Saudi Arabia kuheshimu na kulinda haki za kibinadamu.
Aidha, ameitaka Saudi Arabia kuhakikisha kuna haki na uwazi katika uendeshaji wa kesi.
Kuuawa kwa Sheikh Nimr kulisababisha maandamano maeneo ya Washia Mashariki ya Kati, na hasa Iran na Bahrain.
SaudiImage copyrightGetty
Image captionMaandamano yalifanyika pia mjini Qatif, mkoa wa Mashariki nchini Saudi Arabia
Awali, serikali ya Iran, inayoongozwa na Washia, na ambayo ni mpinzani wa Saudi Arabia inayoongozwa na Wasunni katika kanda hiyo, ilishutumu vikali mauaji ya Sheikh Nimr.
Wizara ya mashauri ya kigeni ya Iran ilisema ufalme huo wa Kisunni utalipia kitendo hicho.
Aidha, ilimwita balozi wa Saudi Arabia mjini Tehran kulalamika.
Kwa upande wake, Saudi Arabia ililalamikia balozi wa Iran kile ilichosema ni uingiliaji kati wa Tehran katika masuala ya ndani ya Riyadh.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni