Breaking News

Jumapili, 8 Novemba 2015

Vita vya Urais Marekani,Republican wachafuana

Ben Carson:Wanahabari wananiharibia jina 





Image copyrightGetty
Image captionBen Carson kushoto

Mmoja wa wagombeaji wa Urais nchini Marekani, aliye mstari wa mbele katika chama cha Republican, Daktari bingwa wa upasuaji aliyestaafu, Ben Carson, ameshutumu vyombo vya habari kwa kile alichosema ni nia yao ya kumchafulia jina.
Tamko lake linatokana na maswali aliyoulizwa kuhusiana na kitabu juu ya maisha yake alichochapisha miaka ya 90 ambapo inasemekana alipewa karo kwenda kusoma katika Shule maalumu ya kijeshi ya West Point.

Sikiliza hii kwa makini, kumbe kuchafuana si Bongo pekee bali hata kwa Obama.

Alisema kuwa hakuomba msaada huo wa karo na wala hakupewa nafasi hiyo na kwamba ripoti zinazochapishwa hivi sasa zinatokana na mazungumzo aliyoyafanya na baadhi ya maafisa wa vyeo vya juu Serikalini.
Mpinzani wake mkuu katika chama cha republican alichapisha habari katika mtandao wa kijamii wa Twitter akisema: "Wau, hiyo ni sehemu ndogo tu ya uongo anaotulimbikizia Ben Carson."

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni