Breaking News

Jumatano, 4 Novemba 2015

Mapigano yazuka Msumbiji

Mapigano mapya kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa chama cha upinzani cha Renamo yameripotiwa nchini Msumbiji.
Polisi wanasema watu kadha wamefariki lakini hawajatoa idadi kamili. Hata hivyo, wamepuuzilia mbali ripoti kwenye vyombo vya habari nchini humo kwamba watu 200 wameuawa tangu wiki iliyopita.
Kiongozi wa Renamo Dhlakama alikataa kutambua matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana
Wasiwasi umekuwa ukiongezeka Msumbiji tangu kusambaratika kwa mchakato wa Amani uliofaa kupelekea kujumuishwa kwa wapiganaji wa Renamo kwenye polisi na jeshi.
Mapigano ya hivi majuzi yalianza wiki iliyopita katikati mwa nchi hiyo eneo ambalo Renamo walikuwa wamejenga kambi ya jeshi hivi karibuni.
Kiongozi mkongwe wa Renamo Afonso Dhlakama amedai serikali ilihusika katika majaribo mawili ya kumuaa, ikiwa ni pamoja na shambulio kwenye msafara wake ambapo watu 24 walifariki. Kuna wasiwasi kwamba mapigano hayo mapya huenda yakaathiri uchumi wa Msumbiji, au hata kutumbukiza taifa hilo kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe tena. chanzo BBC swahili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni