Breaking News

Jumatano, 11 Novemba 2015

My Dady is good on bed than my boyfriend

WAKATI watumishi wa Mungu  na wahubiri mbalimbali wakijaribu kupenyeza ujumbe mzito kuhusu uwepo wa Mwenyezi Mungu katika maisha ya binadamu, Shetani naye hukesha usiku na mchana akijaribu kupenyeza ujumbe wake.

Hata hivyo shetani ameonekana mwenye nguvu zaidi miongoni mwa baadhi ya bianadamu kiasi cha kumfanya binti ama mzazi kufanya mapenzi. Habarimpya.com imefanikiwa kupata mahojiano ya binti mmoja nchini Kenya anyesema kuwa Baba yake ni mzuri kitandani zaidi ya mpenzi wake.

Pata burudani makini ndani ya Habarimpya.com

Mdau wa tovuti ya Habarimpya.com wakati tukiendelea kufanya marekebisho mbalimbali katika tovuti yetu endelea kupata burudani mbalimali.

Leo tunakuletea kibao cha mpita njia kilichoimbwa na mwanadada Allicios Theluji akimshirikisha Juliana Kanyomozi.

Uchambuzi wa magazeti ya leo November 11

Hellow mdau wa tovuti ya Habarimpya.com ni imani yetu kwamba uko salama na unaendelea na majukumu yako katika ujenzi wa taifa.

Hiki ni kipindi cha magazeti, hivyo tunaomba tuungane nawe moja kwa katika luninga ya taifa TBC kupata habari za magazetini.

Jumanne, 10 Novemba 2015

Maalim Seif uso kwa uso na Rais Shein



Zanzibar:Shein akutana na Maalim Seif

  • Saa 5 zilizopita
Image captionRais wa Zanzibar Dokta Ali Mohammed Shein
Mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa visiwani Zanzibar yameendelea huku mkutano uliowaleta pamoja rais Ali Mohammed Shein na kiongozi wa upinzani Seif Sharif Hamad ukifanyika.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, mkutano huo wa faragha katika ikulu ya rais ulihudhuriwa na marais wa zamani Ali Hassan Mwinyi na Amani Abeid karume.
Ni mara ya kwanza kwa Dkt Shein ambaye anatoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Bw Seif wa Chama cha Wananchi (CUF) ambaye ni makamu wa rais wa kisiwa hicho kukutana tangu tume ya uchaguzi kufutilia mbali matokeo ya urais.
Kushirikishwa kwa marais hao wa zamani ni thibitisho kwamba kuna harakati za kisiasa zinazoendelea katika juhudi za kukabiliana na tatizo hilo ambalo limezua mgogoro wa kikatiba.
Wanachama wa jumuiya ya kimataifa pia wanadaiwa kushiriki katika kumaliza tatizo hilo.
Hakuna habari zilizotolewa kutoka pande zote mbili lakini duru za serikali zimethibitisha kwamba mazungumzo hayo yalifanyika kwa faragha.
Image captionMaalim Seif Hamad wa Zanzibar
Makamu wa rais wa pili Seif Ali Idd pia amedaiwa kuhudhuria mkutano huo kulingana na duru hizo.
Bw Mwinyi alikuwa rais wa Zanzibar kwa kipindi kifupi kabla ya kuteuliwa kuwania urais mwaka 1985 huku Karume akiliongoza eneo hilo kutoka mwaka 2000 hadi mwaka 2010.
Maafisa wa ikulu ya rais visiwani Zanzibar hawakuwa tayari kuzungumzia kuhusu yalioafikiwa katika mkutano huo.
Wale kutoka CUF hata hivyo wamesema kuwa majadiliano yalikuwa mazuri kwa maslahi ya raia wa muungano wa Tanzania.

Obama atinga Facebook

Obama hatimaye ajiunga na Facebook

  • Saa 5 zilizopita                                                                         
ObamaImage copyrightAFP
Image captionObama anasema ni muhimu kuhifadhi mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo
Rais wa Marekani Barack Obama hatimaye amejiunga na Facebook, na ujumbe wake wa kwanza umekuwa ni wa kuhimiza watu kuchukua hatua kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Ikulu ya White House kwenye ukurasa huo wake imepakia video ya Obama akitembea katika eneo la South Lawn katika ikulu ya White House.
Hatua yake ya kujiunga na Facebook, mtandao wa kijamii wenye zaidi ya watumiaji bilioni moja, inaonekana kama juhudi za kiongozi huyo kuwafikia zaidi vijana na makundi mbalimbali ya watu.
“Natumai mtachukulia huu kuwa ukumbi ambao tunaweza kutumia kujadiliana kuhusu masuala muhimu kuhusu taifa letu,” anasema kwenye video hiyo.
Obama anaonekana akitembea kwenye bustani hiyo ambayo imekuwa chini yake kwa miaka saba iliyopita, ambayo kama anavyosimulia, ina mbweha, mwewe na vichakuro.
Lengo kuu la kisiasa hata hivyo linaonekana kuhimiza ulimwengu kuunga mkono juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Obama atazuru Paris mwezi Desemba, kutafuta uungwaji mkono wa mkataba wa kuweka vikwazo kwa mataifa kuhusu viwango vya utoaji wa gesi zinazochangia ongezeko la joto duniani.
Kutokana na hali kwamba Bunge la Congress linadhibitiwa na chama cha Republican, ambacho hakijatambua hatari inayotokana na mabadiliko ya tabia nchi, anahitaji kutafuta uungwaji mkono zaidi hata nyumbani.
White House imesema inatumai Facebook itasaidia kama ukumbi wa kubadilishana mawazo.
“Ukurasa huu utawapa Wamarekani jukwaa la kubadilishana mawazo yao na Rais kuhusu masuala ambayo wanayajali sana,” amesema naibu mkurugenzi wa mkakati wa dijitali katika White House Kori Schulman.
Bw Obama alijiunga na mtandao wa kijamii wa Twitter mwezi Mei mwaka huu.

CUF wazidisha utata Zanzibar

Utata wazidi kuhusu mawaziri Zanzibar

Khamis
Image captionBw Khamis amesema kikatiba hakuna mawaziri Zanzibar
Utata umezingira hatima ya mawaziri katika serikali ya visiwani Zanzibar baada ya kuongezewa muda kwa rais wa visiwani kutokana na utata kuhusu matokeo ya uchaguzi.
Chama cha Wananchi (CUF) kimepinga hatua ya kumuongezea muda wa kuhudumu Rais Ali Mohamed Shein anayetoka Chama cha Mapinduzi (CCM) wakisema hatua hiyo haikufuata katiba.
Bw Shein aliongezewa muda baada ya mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi visiwani humo akisema ulijaa udanganyifu.
Lakini chama cha CUF kinasema uchaguzi huo ulikuwa halali na mgombea wake Maalim Seif Sharif Hamad anafaa kutangazwa mshindi.
Mawaziri waliotoka chama cha CUF kwenye serikali iliyofaa kukamilisha muda wake mwanzoni mwa Novemba wamesema kisheria hawamo uongozini.
“Si kwamba tumejiuzulu lakini kisheria na kikatiba muda wetu wa kuhudumu ulimalizika Novemba 2,” amesema Nasor Abubakar Khamis Bakari, aliyekuwa waziri wa haki na masuala ya kikatiba.
“ZEC inafaa kutangaza CUF kuwa mshindi wa uchaguzi kwani hata katika majimbo tayari walitangaza washindi huko.”
Naibu katibu mkuu wa CUF Nassor Ahmed Mazrui, akihutubia kikao cha wanahabari mapema leo mjini Dar es Saaam amesema chama hicho hakijafurahishwa na shughuli inayoendelezwa kwa sasa na ZEC.
Image captionWawakilishi hao wa CUF walikuwa wamebeba vyeti walivyopewa na ZEC
Wawakilishi wateule 27 wa CUF kutoka Zanzibar, walioandamana na baadhi ya viongozi wa chama hicho kwenye kikao cha leo, walisema si haki kwa ZEC kufuta ushindi wao kwa kuwa walishapewa vyeti vya ushindi.

Askari mlarushwa atoa siri za wenzake

Wakati Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Joseph Magufuli, akija na kauli mbiu ya 'hapa kazi', Jeshi la Polisi nchini imeanza kutekeleza kauli mbiu hiyo kwa vitendo.

Jeshi hilo limetekeleza kauli mbiu hiyo kwa kumfukuza kazi aliyekuwa Askari wake kitengo cha Usalama Barabarani Mkoani Tanga kwa tuhuma za kushawishi na kupokea rushwa.