Breaking News

Jumatatu, 14 Desemba 2015

Raia wa Marekani kuondoka Burundi

Serikali ya Marekani imeshauri Raia wake walio nchini Burundi kuondoka nchini humo haraka iwezekanavyo baada ya watu 87 kuuawa kwenye ghasia zilizotokea siku ya Ijumaa.
                                       Siku ya Ijumaa Watu 87 waliuawa mjini Bujumbura 
Ghasia zilizojitokeza kwenye mitaa ya mji mkuu wa nchi hiyo, Bujumbura ni mbaya zaidi tangu kuanza kwa vurugu mwezi Aprili baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuamua kuwania tena urais kwa muhula wa tatu.
Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch (HRW) limeitisha uchunguzi kuhusu mauaji hayo ya Ijumaa.
Mwezi uliopita, Ubelgiji pia iliwashauri raia wake kuondoka Burundi, huku Muungano wa Ulaya (EU) nao ukipunguza wahudumu wake, kwa kuondoa wafanyakazi ambao ni wa muda, "familia na wafanyakazi ambao si muhimu sana."
"Kufuatia machafuko ambayo yanaendelea kuongezeka, Wizara ya Kigeni imeagiza kuondoka kwa jamaa za maafisa wa Marekani na maafisa ambao si wa kushughulikia dharura nchini Burundi," taarifa ya Marekani ilisema.
"Ubalozi wa Marekani unaweza kutoa huduma za dharura kwa kiwango cha chini tu kwa raia wake nchini Burundi."

Jamhuri ya Burundi

Mji Mkuu: Bujumbura

  • Milioni 10.4 Idadi ya watu - sawa na Ubelgiji
  • Kilomita mraba 27,816 Ukubwa - sawa na Haiti
  • Miaka 50 Muda wa kuishi kwa wanaume
  • Miaka 50 Muda wa kuishi kwa wanawake
  • $900 GDP - sawa na Liberia
GETTY IMAGES
Jijini Nairobi, wanaharakati Jumapili jioni waliwakusanya vijana kutoka Burundi, Kenya na nchi nyingine za Afrika Mashariki jijini Nairobi kwa ajili ya mkesha na kuwasha mishumaa kuwakumbuka Raia wa Burundi walioathirika kutokana na mzozo wa kisiasa nchini mwao.
Aidha, walitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni