Wakaazi wa mji wa Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya wanasema wamegundua zaidi ya miili 20 iliyozikwa kwenye makaburi ya jumla.
Miongoni mwa miili hiyo ni ule wa mama mmoja aliyeripotiwa kupotea siku tano zilizopita.
Picha za kusikitisha zilisambaa mitandaonii asubuhi ya leo, zikionyesha sehemu za mwili za watu zikichomoza kutoka makaburi yaliyochimbwa juu juu.
Miili mingine ilikuwa uchi. Mwili wa mama ulioonekana kuharibiwa ulizua hisia nzito zaidi.
Marehemu asemekana alikuwa mama wawatoto watano, aliyekamatwa na watu wasiojulikana siku nne zilizopita.
Seneta wa eneo hilo Billow Kerrow alieleza ugunduzi huo kama wa kutisha, na kudai waliouwawa ni waathirika wa mauaji ya serikali.
Inspekta mkuu polisi Joseph Boinnet alidhibitisha kifo cha mwanamke huyo, lakini akakanusha madai kuwa kuna makaburi ya jumla.
Makundi ya kutetea haki za kibinadamu yanaamini kuwa askari wa kupambana na ugaidi kwa kawaida kuwaua washukiwa.
Aidha wamekashifu vyombo vya usalama kwa kupuuza taratibu za kisheria na kuwaua mashahidi kabla ya kesi zao kumalizika.
Serikali imewahi kuitaja mahakama kama bodi inayovunja guu vita dhidi ya ugaidi.
Mwaka jana Makamu wa Rais William Ruto alisema washukiwa wa ugaidi huachiliwa kwa dhamana kwa urahisi sana wanapofikishwa mahakamani , kisha wao hutoweka wasionekane tena.
Mnamo Mwezi mwei, miili kumi na moja ilipatikana kwenye makaburi mjini wajiri, kusini mwa Mandera.
Mabaki ya risasi yaliyopatikana kando ya makaburi hayo yalizua shauku zaidi kuwa huenda polisi wa kupambana na ugaidi walihusika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni