BBC imebaini kwamba fursa ya kumkamata mtuhumiwa mkuu wa shambulio la mwezi uliopita mjini Paris, nchini Ufaransa huenda imepotezwa. Imethibitishwa kwamba, kulikuwa na jitihada za kimataifa za kumkamata Abdelhamid Abbaoud mjini Athens, mnamo mwezi January.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo alifanikiwa kukwepa mtego huo aliokuwa amewekewa baada ya polisi wa Ubelgiji kusambaratisha mtandao wa kigaidi ambao ulikuwa ukiongozwa na Abdelhamid Abbaoud kutokea katika mji mkuu wa Ugiriki, Athens.
Mtuhumiwa namba moja wa shambulio la kigaidi mjini Paris,Abdelhamid Abbaoud.
Mwandishi wa BBC anaeleza kwamba kushindwa kumkamata mtuhumiwa huyo kumeibua maswali kuhusu kiwango cha ushirikiano kilichopo kati ya mamlaka za usalama katika nchi mbali mbali za umoja wa ulaya. Watu 130 waliopigwa risasi walipoteza maisha katika shambulio hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni