Kasi ya Rais John Magufuli katika kubana matumizi yasiyo ya lazima ya serikali ili fedha zinazookolewa zielekezwe katika kuimarisha huduma za jamii imeendelea kuvutia wengi katika nchi jirani za Afrika Mashariki.
Kasi ya Rais John Magufuli katika kubana matumizi yasiyo ya lazima ya serikali ili fedha zinazookolewa zielekezwe katika kuimarisha huduma za jamii imeendelea kuvutia wengi katika nchi jirani za Afrika Mashariki baada ya jina lake kuanza kutumiwa na wagombea urais nchini Uganda.
Kati ya wagombea wote, aliyejipambanua kwa uwazi kuwa atafuata nyayo za Magufuli katika kuhakikisha kuwa serikali inaendesha mambo yake kwa nia ya kubana matumizi yasiyo ya lazima, kukomesha ufisadi na mwishowe kuwanufaisha watu wa tabaka la chini kupitia uboreshaji wa huduma za jamii ni mgombea wa upinzani anayemtikisa Rais Yoweri Museveni katika kinyang’anyiro hicho, Dk. Kizza Besigye wa chama cha Forum for Democratic Change (FDC).
Katika kampeni zake mwishoni mwa wiki, Besigye amesema wazi kuwa pindi atakapochaguliwa na wananchi na kuingia madarakani, atafuata nyayo za Magufuli kwa kuanza kuipiga bei ndege inayotumiwa na Museveni kwa maelezo kuwa inalibebesha taifa lao gharama kubwa ambazo zinaweza kutumiwa katika kuboresha huduma za jamii.
Besigye alisema yeye anaunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais mpya wa Tanzania, Magufuli, ambaye anaishi kulingana na jina lake la utani la ‘tingatinga’ kutokana na kuchukua hatua kadhaa dhidi ya ufisadi, kuongeza ufanisi wa kazi katika ofisi za umma na pia kuongeza nidhamu ya matumizi kwa manufaa ya taifa na siyo watu wachache.http://www.eatv.tv/news/current-affairs/magufuli-ateka-kampeni-za-urais-uganda
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni