Breaking News

Jumatano, 9 Desemba 2015

Rais Dk Magufuli ,Mkewe wafanya usafi nje ya Ikulu

WAKATI Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Dk John Joseph Pombe Magufuli, akifuta Sherehe za Uhuru zinazofanyika Desemba 9 kila mwaka na kuwataka Watanzania kutumia siku hiyo kufanya usafi katika maeneo yao, kuna baadhi ya watu wametumia siku hiyo kupumzika nyumbani kutokana na hali zao kiafya.


Rais Dk John Magufuli na Mkewe Janneth Magufuli (kulia) wakiwa kwenye aneo la ufuo wa bahari karibu na ikulu wakiwa amevalia glavu kwa ajili ya kufanya usafi. 

Rais Dk Magufuli alifuta Sherehe hizo na kuagiza pesa zinazotumika wakati wa sherehe hizo kuelekezwa katika matumizi mengine, huku wananchi pia wakihimizwa kufanya usafi katika maeneo yao ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu.

Ugonjwa wa kipindupindu umekuwa tishio katika maeneo mbalimbali ya nchi, hususan katika miji ya Dar es Salaam,Mwanza, Mbeya, Iringa ,Morogoro na Arusha. Hata hivyo agizo hilo la Rais limepokelewa kwa kishindo kikubwa, huku wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali za Serikali wakienda kazini kwa lengo la kuungana na jamii kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya miji.



Wanafunzi wa mwaka wa tatu wa chuo kikuu cha Tumaini Iringa wakiwa katika matayarisho ya kufanya usafi kwenye kituo cha mabasi mjini Iringa picha na Maktaba.

Jijini Mwanza watu mbalimbali waliofika mjini kwa shuguli binafsi walijikuta wakikabidhiwa fagio kwa nguvu na kufanya usafi mara tu wanaposhuka kwenye vyombo vya usafiri. Watu wengine walioungana na jamii kufanya usafi ni pamoja na Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, Gloria Ndosi ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa. Akizungumza na tovuti hii kwa njia ya simu amesema kwamba, agizo la Rais limepokelewa vizuri.

"Mimi ni muumini mzuri wa masuala ya usafi, napenda kuishi , kusoma na kufanyakazi katika mazingira ya usafi, ndiyo maana nimeamka mapema kufika maeneo ya Chuo na kuuungana na wanachuo wenzangu kufanya usafi, kwanza nilidhani nitakuwa peke yangu lakini nikashangazwa na muitikio wa watu ,nimekuta watu wengi wanafanya usafi , kwakweli ni jambo la kumpongeza Rais kwa hatua hii"alisema Ndosi. Hii ni mara ya kwanza kwa Sherehe hizo kufutwa tangu nchi hii ilipopata Uhuru mwaka 1961 Desemba 9. Imeandikwa na Waandishi Wetu, Dar es Salaam, Iringa na Mwanza.

Maoni 1 :

  1. Maisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma,

    Kwaheri Gerd Ulrich

    JibuFuta