Breaking News

Ijumaa, 6 Novemba 2015

Ungana nasi katika uapisho wa Rais Magufuli

1.12pm:Sasa rais Magufuli akiandamana na mkewe wanaondoka katika uwanja wa Uhuru baada ya kuapishwa rasmi.
1.09pm:Amewataka viongozi wa upinzani kushirikiana na serikali yake akisisitiza kuwa uchaguzi umekwisha na kwamba rais aliyechaguliwa ni John Pombe Magufuli

  Rais wa Serikali ya awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Makamu wake Mama Samia Suluu,baada ya kuapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania 
1.06pm:Magufulu aipongeza tume ya uchaguzi kwa kufanya uchaguzi ulio huru mbali na vyombo vya usalama vilivyoimarisha amani.Awashukuru wanahabari kwa kuwaelimisha raia wa Tanzania
1.05pm:'Sasa ni kazi tu' awataka viongozi wa upinzani kushirikiana kwa lengo la kuendeleza na kuwahudumia watanzania
1.04pm:''Nashukuru wagombea wanzangu kwa kutupa chanagmoto,tumejifunza mengi kutoka kwao''.
1.03pm:''Natambua kwamba nina jukumu kubwa la kuwafanyia kazi watanzania,lakini hatahivyo tumuweke mungu mbele ili kutekeleza ahadi hizo.
1.02pm:Magufuli:Nawashkuru watanzania kwa kunichagua kwa kura nyingi ili kuongoza taifa kwa miaka mitano ijayo.
1.01apm:Magufuli:Nawashukuru viongozi mbali,mbali waliowasili hapa ili kujumuika nami katika sherehe hii muhimu.
1.00pm:Namshkuru sana mwenyezi mungu aliyetujalia kuwepo hapa pamoja na viongozi wa dini.
12.58pm:Na sasa ni wakati wa rais John Pombe Magufuli kulihutubia taifa.

 Viongozi watambulishwa kwa umati,Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe,wapili kulia,Rais wa Rwanda Paul Kagame kushoto,Rais wa DR Congo Raurent Kabila kulia,Rais wa Kenya Uhuru Kenyata wa tatu kulia.
12.06am:Marais na viongozi mbalimbali waliowasili katika hafla hiyo watambulishwa kwa wananchi waliojaa katika uwanja huo.

Rais Magufuli akipigiwa mizinga 21, kama ishara ya kukaribishwa katika utawala mpya wa nchi.
12.00am:Na sasa kamanda wa jeshi anaomba rukhsa ya kuondoka uwanjani.

Rais wa awamu ya tano John Pombe Magufuli kulia, akiwa na rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete, wakipokea salamu za utii kutoka kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Genali Davis Mmwamunyange kulia na mlinzi wa rais kushoto.
11.56am:Ndege za kijeshi zinapita juu ya uwanja wa Uhuru kutoa heshima kwa rais mpya wa taifa hilo John Pombe Magufuli.
11.27am:Rais Magufuli alikagua gwaride la heshima
11.23am:Mizinga 21 ya kumkaribisha rais mpya wa Tanzania John Pombe Magufuli yapigwa
11.22am:Jeshi laomba rukhsa kutoka kwa rais mpya wa Taifa la Tanzania John Pombe Magufuli

                                                             Jukwaa la kula kiapo
11.20am:Jakaya Mrisho Kikwete sasa awasalimia viongozi waliofika katika jukwaa la waheshimiwa wakiwemo marais mbalimbali.

Rais aliyemaliza muda wake,Jakaya Mrisho Kikwete,kushoto akiwa na aliyekuwa makamu wake Dk Mohamed Garrib Bilal,wakiondoka Uwanjani kwa gari la wazi kama ishara ya kuachia madaraka kwa serikali mpya.
11.18am:Sasa jeshi lamuaga aliyekuwa rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete na aliyekuwa makamu wake Gharib Bilal
10.55am:Makamu wa rais wa Kwanza mwanamke nchini Tanzania Samia Suluhu Hassan aapishwa

Rais Dk John Pombe Joseph Magufuli,akionyesha slaa za jadi za asili ya mtanzania kama ishara ya kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wa Tanzania
10.51am:Rais mpya wa Tanzania apewa mkuki na ngao ya ishara ya kuchukua madaraka.
10.48am:''Mimi John Pombe Magufuli naapa nitatenda kazi zangu za urais kwa mujibu wa sheria na mila na desturi za muungano wa Tanzania,ewe mwenyezi mungu nisaidie''
10.47am:Rais mteule John Pombe Magufuli aapisshwa .Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pia amewasili hapa.

      Bendera ya Rais Kikwete ikishushwa kuashiria mwisho wa utawala wake.
10.45am:Na sasa aliyekuwa rais wa taifa hilo Jakaya Kikwete amekuwa raia wa kawaida baada ya bendera ya utawala wake kushushwa hapa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
10.40am:Wimbo wa Taifa la Tanzania wapigwa na baadaye bendera ya rais Kikwete itashushwa ili kuashiria mwisho wa uoingozi wake.

              Rais Jakaya Kikwete,akipigiwa mizinga 21 ya mwisho katika utawala wake
Mizinga 21 ya kutoa heshima za mwisho kwa rais Jakaya Kikwete yapigwa.

                                             Kikwete akizunguka uwanja
10.21am:Gari la gwaride la kijeshi lililombeba rais Kikwete sasa lauzunguka uwanja huo huku wananchi waliojjaawa na furaha wakimsalimia kwa kumpungia mkono.
10.20am:Na sasa msafara wa Rais Jakaya Kikwete wawasili katika uwanja wa Uhuru .KIkwete baadaye anaonekana kuingia katika gari rasmi la gwaride katika uwanja wa uhuru na kuwapungia mkono maelfu ya wananchi waliojaa katika uwanja huo.
10.15am:Rais Mteule John Pombe Magufuli awasili katika sherehe hizo na kulakiwa na jaji mkuu Othman Chande.

                                                              Uwanja wa Uhuru
9.48am:Rais wa Rwanda Paul Kagame anawasili katika uwanja wa uhuru na kuketi bega kwa bega na waliokuwa marais wa taifa hilo Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.
9.47am:Rais wa kisiwa cha Zanzibar Dokta Ali Mohammed Shein amewasili katika uwanja wa Uhuru na anaonekana hapa akisalimiana na rais mstaafu wa Tanzania Hassan Mwinyi.Kumbuka kiongozi huyo wa Zanzibar aliongezewa mda wa kuhudumu katika kisiwa hicho baada ya tume ya uchaguzi kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais katika kisiwa hicho.
9.43am:Rais mteule John Pombe Magufuli atakuwa rais wa awamu ya tano kuchaguliwa nchini Tanzania tangu taifa hilo lijipatie Uhuru.

                                                      Raia waliowasili uwanjani
9.39am:Vilevile aliyekuwa waziri mkuu nchini Kenya Raila Odinga ambaye ni rafiki mkubwa wa rais mteule John Pombe Magufuli,rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph kabila pamoja na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ni baadhi ya viongozi waliowasiliili kuhudhuria sherehe hiyo ya kihistoria.
9.35am:Miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa katika hafla hii ni pamoja na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye tayari ameondoka katika uwanja wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi akiandamana na Mkewe bi. Margeret Kenyatta na anatarajiwa kuwasili katika uwanja wa sherehe hizi wakati wowote kutoka sasa
9.30am:Gwaride la kijeshi tayari limejiandaa vilivyo ikiwemo wanajeshi waliovalia sare za rangi tofauti hapa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

                                                                     Mapambo
8:00 am Mataifa mbalimbali yamekuwa yakituma risala za pongezi kwa Tanzania na kwa Rais Mteule John Magufuli.
Wa kwanza kutuma risala za pongezi walikuwa ni:
Rais wa Rwanda Paul Kagame na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Saharawi Mohammed Abdelaziz.
Katika salamu zake kwa Rais Mteule Magufuli, Bw Kagame amesema: "Kufuatia kuchaguliwa kwako kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, napenda kukutumia Mheshimiwa salamu za dhati, pongezi na heri nyingi kwa niaba yangu mwenyewe, Serikali yangu na wananchi wa Rwanda.”
Naye Rais Abdelaziz amemwambia Rais Mteule Magufuli: “Sisi tuna uhakika kuwa chini ya uongozi wako wa busara, Tanzania itaendelea kusonga mbele na kupata maendeleo na ustawi mkubwa zaidi.”
7:10 am Viongozi wa baadhi ya mataifa ya Afrika wanatarajiwa kuhudhuria wakiwemo Jacob Zuma kutoka Afrika Kusini, Robert Mugabe kutoka Zimbabwe na Filipe Nyusi wa Msumbiji. Mhubiri mashuhuri kutoka Tanzania TB Joshua pia atahudhuria sherehe hiyo.
7:00 am Watumbuizaji wanaotarajiwa kutumbuiza wakati wa sherehe walifika uwanjani mapema na ala zao.

6:45 am Uwanja umeanza kujaa watu. Wengi wa waliofika mapema wanafurahisha kujipiga, kupigana na kupigwa pichwa kuweka kama kumbukumbu za siku hii.

Image caption Baadhi ya waliofika wamevalia mavazi yenye rangi za chama tawala CCM

6:30 am Uwanja wa Uhuru umepambwa ukapambika

                                                 Uwanja wa Uhuru

6:30 am Waandishi wa BBC wamo katika uwanja huo kukuletea habari kadiri zinavyochipuka.

Mubali
                                       Mwandishi wa BBC Leonard Mubali

6:30 am Sherehe ya kumuapisha Bw Magufuli inafanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

                       Usalama umeimarishwa katika uwanja huo
6:00 am. HABARI YA ASUBUHI?
Rais Mteule wa Tanzania John Pombe Magufuli anaapishwa leo kuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 25.
Rais Magufuli alipata asilimia 58.46 ya kura zilizopigwa kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania. chanzo BBC/Swahili

Jumatano, 4 Novemba 2015

Mapigano yazuka Msumbiji

Mapigano mapya kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa chama cha upinzani cha Renamo yameripotiwa nchini Msumbiji.
Polisi wanasema watu kadha wamefariki lakini hawajatoa idadi kamili. Hata hivyo, wamepuuzilia mbali ripoti kwenye vyombo vya habari nchini humo kwamba watu 200 wameuawa tangu wiki iliyopita.
Kiongozi wa Renamo Dhlakama alikataa kutambua matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana
Wasiwasi umekuwa ukiongezeka Msumbiji tangu kusambaratika kwa mchakato wa Amani uliofaa kupelekea kujumuishwa kwa wapiganaji wa Renamo kwenye polisi na jeshi.
Mapigano ya hivi majuzi yalianza wiki iliyopita katikati mwa nchi hiyo eneo ambalo Renamo walikuwa wamejenga kambi ya jeshi hivi karibuni.
Kiongozi mkongwe wa Renamo Afonso Dhlakama amedai serikali ilihusika katika majaribo mawili ya kumuaa, ikiwa ni pamoja na shambulio kwenye msafara wake ambapo watu 24 walifariki. Kuna wasiwasi kwamba mapigano hayo mapya huenda yakaathiri uchumi wa Msumbiji, au hata kutumbukiza taifa hilo kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe tena. chanzo BBC swahili

Rais Kikwete,Maalim Seif uso kwa uso

Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania amefanya mazungumzo na makamu wa rais wa kwanza kisiwani Zanzibar ambaye ndiye mgombea Urais kupitia tiketi ya chama cha upinzani (CUF) Maalim Seif katika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo inajiri wakati ambapo kuna mkwamo wa kisiasa kisiwani humo baada ya Tume ya Uchaguzi(ZEC) kufuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika .
Hatahivyo mwandishi wetu aliyezungumza na mkurugenzi wa maswala ya mawasiliano katika chama cha CUF amesema kuwa hakuna lolote la muhimu lililoafikiwa isipokuwa 'mazungumzo ya kawaida'.
Amesema kuwa wamehuzunika baada ya kubaini kuwa rais Jakaya Kikwete anakamilisha muhula wake wa uongozi hapo kesho.

Real Madrid na Man City zapeta UEFA

Real Madrid na Manchester City zimefuzu kwa hatua ya muondoano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kupata ushindi mechi zilizochezwa Jumanne. Wakati Real Madrid ikipata ushindi mwembamba kwa kuifunga Paris Saint Germain goli 1 - 0. Manchester wao walishusha kipigo kwa Sevilla cha 3 -1.
Matokeo kamili haya chini.
Real Madrid 1 - 0 Paris St Germain
Man Utd 1 - 0 CSKA Moscow
FC Astana 0 - 0 Atl Madrid
Sevilla 1 - 3 Man City
Shakt Donsk 4 - 0 Malmö FF
PSV Eindhoven 2 - 0 VfL Wolfsburg
Benfica 2 - 1 Galatasaray
Borussia M'gladbach 1 - 1 Juventus

TB Joshua atua Tanzania

Mhubiri mashuhuri kutoka Nigeria TB Joshua ni miongoni mwa wageni mashuhuri watakaohudhuria sherehe ya kumuapisha John Pombe Magufuli kuwa rais mpya wa Tanzania Alhamisi.
Bw Joshua ambaye ni mhubiri wa kanisa la Church of All Nations aliwasili jijini Dar es Salaam Jumanne. Baada ya kuwasili kwa mhubiri huyo, Bw Magufuli aliandika kwenye Twitter: "Tumshukuru Mungu, tumepata ugeni wa Nabii TB Joshua, atashiriki nasi katika sherehe nitakapoapishwa kuwa Rais wa awamu ya Tano wa Tanzania."
                                          TB Joshua alimtembelea Rais Kikwete ikuluni Dar es Salaam 
Baadaye, alikutana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika ikulu ya Dar es Salaam. Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, ambaye ni rafiki wa karibu wa Bw Magufuli, pia anatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo.
Tayari muungano wa Cord unaoongozwa na Bw Odinga umeahirisha shughuli ya kuwasilisha sahihi za kuunga mkono marekebisho ya katiba kwa Tume ya Uchaguzi ya Kenya (IEBC) ili kuhudhuria sherehe hiyo. Muungano huo ulikuwa awali umepanga kuwasilisha sahihi hizo leo.
Bw Magufuli, aliyekuwa mgombea wa chama tawala cha CCM ataapishwa kuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada yake kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Novemba 25, matokeo ambayo yalipingwa na chama kikuu cha upinzani nchini humo Chadema.
Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Chadema Edward Lowaasa aliibuka wa pili, kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania. Chanzo BBC Swahili

Wazazi wa mtoto huyu wanatafutwa

Picha hii ya mvulana anayeonekana kujiuliza maswali si haba akilini mwake akiwa na Mzungu imesambazwa mara nyingi sana mtandaoni.Wengi wamekuwa wakiitumia kukejeli vyombo vya habari, mataifa na mashirika ya kutoa misaada kutoka Magharibi kwa mtazamo wao kuhusu Afrika. Kunao wanaoitumia hata hivyo kuuliza maswali ya kijumla tu.

                       Wengi wameitumia kukejeli mtazamo wa nchi za Magharibi kuhusu Afrika 

Lakini je, wajua picha hii ilitoka wapi? Mvulana huyu ni nani?
Picha hii ilianza kuenea sana mtandaoni baada ya kupakiwa kwenye tovuti ya Reddit miaka mitatu iliyopita na mwanamume kutok Texas, Marekani aliyevutiwa nayo baada ya kuiona kwenye ukurasa wa Facebook wa rafiki yake.

Mwanamke aliye kwenye picha hiyo ni Heena Pranav, daktari mwenye umri wa miaka 28 anayeishi Chicago.
Mwaka 2012, alipokuwa mwanafunzi, alizuru mji wa Gulu, kaskazini mwa Uganda kusaidia kwenye mradi wa kuwasaidia wanawake walioathiriwa na vita vya wapiganaji wa Lords Resistance Army. Mradi huo ulisimamiwa na shirika laPros for Africa, linaloongozwa na mtawa Mkatoliki, Rosemary Nyirumbe.
Picha hiyo haikuhusiana na mradi huo na Pranav, akizungumza na BBC Trending radio, amesema alikutana na mvulana huyo sokoni na anakadiria alikuwa na umri wa miaka miwili au mitatu.
"Nilikuwa na wanafunzi wengine wakati huo, na tulikuwa tunapiga gumzo na nikaona mvulana mdogo, aliyenivutia sana,” Pranav alisema.

Picha hii ilianza kuvuma sana baada ya kupakiwa katika mtandao wa kijamii wa Reddit 
“Mamake alikuwa karibu akifanya kazi sokoni. Nilimwendea mvulana huyo kumsalimia na kucheza naye … alikuwa mchangamfu sana."
Mvulana huyo hakuzungumza Kiingereza, na Pranav naye haelewi lugha za wenyeji. Lakini mkutano wao mfupi ulinakiliwa kwenye picha iliyopigwa na mmoja wa wanafunzi kwenye kundi la Pranav. Binti huyo anasema hakuwa amewahi kusikitia Reddit hadi pale rafiki yake alipoipakia picha hiyo huko na ikasambaa sana.
"Sikudhani hili lingelitokea,” anasema. “Kungelikuwa na uwezekano ningetaka sana mtoto huyu na mamake wajue kuhusu haya na wanufaike kiasi kutokana nayo, kwa sababu nadhani alitumiwa bila kupata manufaa yoyote.”BBC Trending inamtafuta mtoto huyu, kwa hivyo iwapo unamfahamu au unajua familia yake, tutumia barua pepe kupitia trending@bbc.co.uk.

Jumapili, 1 Novemba 2015

Hii ndiyo Tanzania mpya

Rais Mteule wa awamu ya tano,Dk.John Pombe Magufuli akionyesha hati ya utambulisho ya ushindi wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyopewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC),Jaji Damiani Lubuva (kulia).

Tukio hilo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali,mabalozi,viongozi wa dini,wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wageni waalikwa  katika Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Makamu wa Rais Mteule,Samia Hassan Suluhu na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa tume hiyo,Ramadhani Kailima. Picha na Elisa Shunda