Breaking News

Ijumaa, 30 Oktoba 2015

Moja kwa moja: Magufuli akabidhiwa cheti Tanzania




Msafara wa Bw Magufuli umelindwa vikali na maafisa wa usalama
11:30am: Msafara wa Rais mteule John Magufuli pamoja na ule wa Rais Jakaya Kikwete waelekea ikulu chini ya ulinzi mkali.



Anna Mghwira akimpongeza Magufuli
11:00am: Mgombea urais wa chama cha ACT Wazalendo Anna Mghwira aliyemaliza wa tatu ni miongoni mwa waliofika kumpongeza Bw Magufuli.



 
11:00am: Rais anayeondoka Jakaya Mrisho Kikwete amehudhuria hafla hiyo, sawa na kiongozi wa ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa Jumuiya ya Madola Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan. Bw Jonathan amampongeza rais mteule.



 
11:10am: John Pombe Joseph Magufuli akabidhiwa rasmi cheti cha ushindi uchaguzi wa rais uliofanyika Jumapili Oktoba 25.




 
11:00am: Hafla ya kumkabidhi Magufuli cheti inafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.Ukumbi huo umejaa watu hadi pomoni.



 
10:20am: Jeshi la Tanzania limeonekana likisafirisha magari ya kijeshi, wanajeshi na silaha hadi visiwani Zanzibar. Matokeo ya uchaguzi visiwani humo yalifutiliwa mbali na mwenyekiti wa tume Jecha Salim Jecha.
9.00am: Mgombea urais wa chama cha CCM John Magufuli leo anakabidhiwa cheti cha ushindi na tume ya uchaguzi baada yake kutangazwa mshindi Alhamisi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema kuwa Magufuli, alijipatia kura 8,882,935 ikiwa ni aslimia 58.46.
Mpinzani wake wa karibu Edward Lowassa wa chama cha Chadema alijipatia kura 6,072,848 ikiwa ni asilimia 39.97 ya kura zote halali.
Baada ya kutangazwa kwa ushindi wake, wafuasi wake walisherehekea katika miji mbalimbali nchini humo. chanzo BBC Swahili

Ndugu wadau na wasomaji wa tovuti ya Habarimpya.com ,Kampuni ya Japo Investment Network inayomiliki mtandao wa Habarimpya.com inaomba radhi kwa mtandao huo kutokuwa hewani tangu leo asubuhi ,kutokana na sababu ambazo ziko nje ya uwezo wetu.

Ingawa wataalum wetu wa masuala ya IT wanaendelea kutatua sababu hizo, tumeamua kuwaletea tovuti nyingine ya www.Habarimpya-tz.blogspot.com.
Kupitia tovuti hii mtaendelea kupata taarifa zote za muhimu kutoka nje na ndani ya nchi, poleni sana kwa usumbufu na karibu sana.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni