Breaking News

Ijumaa, 30 Oktoba 2015

Maoni ya mdau kupitia Facebook

Sina tatizo na ushindi wa urais wa Magufuli, ninachowalaumu wa Watanzania ni uamuzi wao wa kujaza wa Wabunge wengi wa CCM katika chombo muhimu cha uamuzi wa nchi hii.
Kitendo cha Watanzania kuwachangua zaidi wabunge 177 wa CCM ni wazi zile ndiyooo ambazo hazina tija zitaendelea kutawala zaidi na mambo mengi ya kitaifa yatakwama kwa sababu ya kosa hili.

Sioni jinsi mafisadi watakavyoweza kupelekwa katika mahakamani.
Lakini kwa sababu ujinga wetu tumeamua kumpa Magufuli wabunge wake wengi basi tujiandaa. Mungu ibariki Tanzania,  Andrew Kingamkono
Naamini Magufuli angefanya kazi kwa kasi zaidi kama angekuwa na idadi kubwa ya wabunge kutoka upinzani, lakini kwa hali ilivyo sasa, sioni jinsi Katiba ya wananchi itakavyoweza kurudishwa na kuheshimiwa, sioni jinsi mikataba mibovu ya madini itakavyojadiliwa kwa uwazi bungeni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni