Breaking News

Ijumaa, 30 Oktoba 2015

John Magufuli CCM 8,882,935 58.46

 
Magufuli alikuwa Waziri wa Ujenzi katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete anayeondoka mamlakani

Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha CCM John Pombe Magufuli ndiye rais mteule wa taifa la Tanzania baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumapili.
 
Akitoa matokeo hayo mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa Magufuli, ambaye alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa leo, alijipatia kura 8,882,935 ikiwa ni aslimia 58.46 huku mpinzani wake wa karibu Edward Lowassa wa chama cha Chadema akijipatia kura 6,072,848 ikiwa ni asilimia 39.97 ya kura zote. Dkt Magufuli alizaliwa Oktoba 29, 1959.
Haya ndiyo matokeo kamili kama yalivyotangazwa na Jaji Lubuva:
Matokeo ya uchaguzi wa urais Tanzania
Jina Chama Kura Asilimia
Anna Mghwira ACT 98,763 0.65
Chifu Yemba ADC 66,049 0.43
John Magufuli CCM 8,882,935 58.46
Edward Lowassa CHADEMA 6,072,848 39.97
Hashim Spunda CHAUMA 49,256 0.32
Janken Kasambala NRA 8,028 0.05
Macmillan Lyimo TLP 8,198 0.05
Fahmi Dovutwa UPDP 7,785 0.05

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni