Breaking News

Ijumaa, 30 Oktoba 2015

Magufuli apewa cheti cha ushindi Tanzania

Mgombea urais kupitia chama cha CCM John Mafuguli amepewa cheti cha ushindi baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumapili. Bw Magufuli amekabidhiwa cheti hiyo kwenye hafla iliyoandaliwa katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo imehudhuriwa na kiongozi anayeondoka mamlakani Rais Jakaya Kikwete pamoja na waangalizi wa uchaguzi kutoka makundi mbalimbali.

                    Tume ya uchaguzi ilisema Magufuli alipata asilimia 58.46 ya kura zilizopigwa  

 Kadhalika, mgombea wa pekee mwanamke katika kinyang'anyiro hicho Bi Anna Mghwira wa chama cha ACT Wazalendo alihudhuria hafla hiyo, na kumpongeza Bw Magufuli kwa ushindi wake.
Kiongozi huyo mpya hakutoa tamko lolote wakati wa hafla hiyo na alifululiza moja kwa moja hadi ikulu chini ya ulinzi mkali.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema Alhamisi kuwa Magufuli, alijipatia kura 8,882,935 ikiwa ni asilimia 58.46. Mpinzani wake wa karibu Edward habarimpya.comLowassa wa chama cha Chadema alijipatia kura 6,072,848 ikiwa ni asilimia 39.97 ya kura zote halali.

Matokeo hayo yamepingwa na Bw Lowassa na chama chake.
Akiwahutubia wanahabari kabla ya kutangazwa kwa matokeo Bw Lowassa alidai tume imeshirikiana na chama tawala kumpokonya ushindi. Aliitaka tume hiyo kumtangaza kuwa mshindi.
Lakini tume hiyo imejitetea na kusema mchakato wote ulikuwa huru na wa haki na kwamba uliendeshwa kwa kufuata katiba. Bw Magufuli, ambaye alikuwa Waziri wa Ujenzi katika serikali ya Rais Kikwete, anatarajiwa kuapishwa kuwa rais katika muda wa siku saba zijazo. chanzo BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni