Breaking News

Jumamosi, 2 Januari 2016

Safari za Treni zasitishwa Tanzania

KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE)
UONGOZI WA TRL WASIMAMISHA HUDUMA ZAKE BAADA YA ENEO LA KILOSA HADI GULWE KUKUMBWA NA MAFURIKO
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania TRL umetangaza kusitisha kwa muda kuanzia jana Januari 01, 2016, huduma zake baada ya eneo la reli ya kati ya Kilosa mkoani Morogoro na Gulwe mkoani Dodoma tuta la reli kukumbwa na Mafuriko.
Kwa mujibu wa taarifa za kifundi eneo lililoathiriwa na mafuriko ni kubwa hivyo Wahandisi na Mafundi wa TRL wako eneo la mafuriko kutathmini ukubwa wa kazi yenyewe.
Kutokana na uamuzi huo treni ya abiria kutoka bara ilibidi safari yake ikatizwe ilipofika Dodoma na tayari utaratibu unaandaliwa wa kupata mabasi 17 kuwasafirisaha hadi Dar es Salaam abiria 1,119 . wa treni hiyo.
Hali kadhalika kwa vile tarahe ya kuanza tena huduma bado haijaujulikana, safari zote kuanzia jana Januari 01, 2016, kwenda bara zimefutwa na abiria husika wametakiwa kufika katika vituo vya reli walikokata tiketi ili warejeshewe fedha zao na kupata fursa ya kutafuta usafiri mbadala.
Aidha imesisitizwa kuwa Uongozi kwa wakati muafaka itatoa taarifa kamili kuhusu lini huduma za TRL kwenda bara zitaanza tena.
Wito unatolewa kwa kila mwananchi atakayepata taarifa hii muhimu amwaarifu mwenzake.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Elias Mshana.
Dar es Salaam,
Januari 02, 2016

Ijumaa, 1 Januari 2016

Rais Pombe,amtembelea Kadinali Pengo Hospitalini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki la Dar es salaam.

Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo alielazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo January 1, 2016.

 Kardinali Pengo alilazwa hospitalini hapo jana jioni kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.  - See more at: http://asaliwamoyo.blogspot.com/2016/01/habari-hivi-punde-tukio-kubwa-latokea.html#sthash.PgAN6bDs.dpuf

Jumatatu, 14 Desemba 2015

Rais Jammeh atangaza Gambia kuwa nchi ya Kiislamu

Rais wa Gambia Yahya Jammeh ametangaza taifa hilo lenye Waislamu wengi kuwa jamhuri ya Kiislamu, hatua ambayo anasema inakatiza kabisa uhusiano na historia ya zamani ya kikoloni.
Bw Jammeh ameambia runinga ya taifa kwamba tangazo lake linaambatana na sifa na maadili ya kidini ya Gambia.
Jammeh aliondoa Gambia kutoka Jumuiya ya Madola 2013
Ameongeza kuwa raia na wageni wa dini nyingine hawatalazimishwa kuvalia mavazi ya Kiislamu, na wataruhusiwa kuendelea na dini zao bila kusumbuliwa. Asilimia 90 ya raia wa Gambia ni Waislamu.
Koloni hiyo ya zamani ya Uingereza hutegemea sana utalii. Uhusiano kati ya taifa hilo na nchi za Magharibi umekuwa ukidorora siku za karibuni.
Muungano wa Ulaya ulikatiza kwa muda pesa za msaada kwa Gambia mwaka jana kutokana na rekodi mbaya ya haki za kibinadamu. Bw Jammeh ameongoza taifa hilo ndogo la Afrika Magharibi kwa miaka 21.
Mataifa mengine yanayojitambulisha kama jamhuri za Kiislamu ni Iran na Pakistan, na barani Afrika kuna Mauritania.
Bw Jammeh aliondoa Gambia kutoka kwa Jumuiya ya Madola 2013 akitaja muungano humo kuwa wa ukoloni mamboleo. Mwaka 2007, alidai kuwa alikuwa amepata dawa ya kiasili ambayo ingetibu Ukimwi.Source BBC/Swahili

Sumaye,Lowassa,Kingunge ni Chatu mbele ya Mbwa

Na Thadei Ole Mushi.
Nilishawahi kukaa na wawindaji walinihadithia hadithi moja kuwa Mbwa hujipeleka kwa chatu mwenyewe angali akijua anaenda kumezwa. Wawindaji hawa waliniambia kuwa Chatu amuonapo Mmbwa hutoa harufu moja ambayo mbwa huipenda kweli na mbwa humfuata Chatu mwenyewe na kumezwa. Wakati mbwa akimfuata chatu huenda akilia kwani anajua kinachoenda kumkuta mbeleni.
Kisa hiki nimekikumbuka ninavyona Chadema kinavyowapokea kina Sumaye. Najua wanajua madhara ya kuwapokea watu wenye makando kando ila kuna harufu watu hawa wanaitoa na inawavutia kina Mbowe. Hivyo wanawapokea ila najua Moyoni mwao kuna manunguniko makuu.
Ili hili Taifa liendelee kwa kasi linahitaji pia upinzani wenye tija na upinzani wenye nguvu. Sijui kama nyie wenzangu mnaona haya ninayoyaona mimi kuhusu chama cha CHADEMA , ambacho kimeendelea kukipa changamoto chama changu na kukifanya kufanya kazi na usiku. Naamini pia bila CHADEMA hakuna pia CCM imara, CHADEMA wanafanya kazi ya (watch dog) kila mtu akipotoka ndani ya serikali CHADEMA kinapaza sauti na Kumrudisha kwenye mstari. Ndio Maana nahitaji pia CHADEMA kikue na kiwe na uwezo hata wa Kuchua dola ili kiwe mbadala wa CCM baadaye.
Jana nimesikia aliyekuwa waziri mkuu mstaafu kahamia Chadema na kupewa kadi ya chama na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe. Mimi sina tatizo na Chadema kupata wanachama wapya ila nina tatizo na aina ya wanachama wenyewe wanaohamia kwa sasa.
Tumeona faida na hasara za Lowassa kuhamia chadema, ni kweli kuwa Lowassa amekisaidia chama kwa upande mmoja kuongeza wabunge na hata ruzuku najua itaongezeka. Wakati unahesabu faida ya ujio wa Lowassa pia uhesabu na hasara yake kuhamia ndani ya Chadema.
Ni ukweli kwamba Chadema kwa sasa kimekosa hoja ya kujinasibu nayo kisiasa. Kama nilivyowahi kusema agenda ya UFISADI ilikuwa ndio agenda iliyokikuza chama hicho ila kwa sasa hawana tena hoja hiyo kutokana na waliowatukana na wanaotuhumiwa kwa ufisadi ndio wanakiongoza chama.
SUMAYE, LOWASSA NA KINGUNGE UGONJWA UTAKAOKIFUTA CHADEMA KABISA KWENYE RAMANI ZA SIASA.
Hawa kwa pamoja ni wanasiasa wanaounganishwa na agenda moja tu yenye malsahi kwao nayo ni "URAISI" ukiondoa agenda ya uraisi miongoni mwa watu hawa ni maadui wa kutupwa. Maslahi ndio yanayowaunganisha na sio itikadi za chama au hawakujiunga CHADEMA kwa kuwa wanavutiwa na sera za CHADEMA la Hasha!!!.
Sumaye ameamua rasmi kuhamia jana Chadema kwa kuwa ameona uchochoro wa kutimiza ndoto zake za kuwa raisi wa nchi hii baadaye.
Sumaye anajua fika kuwa baada ya miaka 5 Lowassa hatakuwa na nguvu aliyonanyo hivyo chama kitampa nafasi ya kugombea. Hili ni hatari kama Lowassa ataendelea kuimarika kiafya kama nilivyomuona kwenye msiba wa Mawazo. Kama hali ya Lowassa itaendelea hivi hatakubali kunyanganywa nafasi ya kugombea na tukumbuke kuwa Lowassa nje ya chadema ni taasisi inyaojitegemea chini ya 4U Movement.
Kitakachotokea kuanzia sasa ni Lowassa na Sumaye kuendelea kujijenga kila mmoja kwa style yake huku jicho na fikra za kila mmoja wao zikilenga 2020 na sio kukisaidia Chama kujijenga kama Taasisi, baadaye kwenye mchakato wa kumpata mtu wa kukiwakilisha chama kwenye nafasi ya uraisi kila mmoja atataka awe yeye na watapasuka na chama kitakosa mwelekeo. Kama watu hawa hawatadhibitiwa sijui kama chama kitaweza kuhimili mpasuko wake baadaye.
Watu hawa pia wanazuia watu wenye vipaji vya uongozi na wenye uwezo zaidi ndani ya Chadema kupata nafasi ya kugombea Uraisi. Hata aje Malaika ndani ya chadema akataka kugombea Uraisi mbele ya Sumaye na Lowassa hawatapewa nafasi. Pia wanazuia watu wasafi kujiunga na Chadema kwani watahesabiwa kuwa fungu moja la wachafu. Ni aibu kwa chama kama chadema leo kuogopa kuukemea ufisadi.
CHADEMA wanapaswa kufungua macho hapa na kuwadhibiti watu hawa. Aidha makandokando yao yatakichafua pia chama ni bora Sumaye angehamia NCCR kwa kuwa kipo ndani ya Ukawa mchango wake bado ungeonekana. Chukua makando kando ya sumaye changanya na ya Lowassa halafu usisahau agenda waliyoibeba kichani sioni CHADEMA ikipona.
Tuvute subira wale vijana wasiotaka kufikiri ni ruksa kutukana kwani ndio malezi wanayopata huko waliko.
OLE Mushi

Floyd Mayweather Buys $400k On A Mink Coat

Floyd Mayweather Buys $400k On A Mink Coat

CCM imeshinda majimbo manne kati ya matano

Mpaka sasa jumla ya Majimbo 5 yamefanya uchaguzi kati ya Majimbo 7 ya Tanzania Bara na 1 la Zanzibar ambayo hayakufanya uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali Tarehe 25 October 2015.
1. LULINDI-MTWARA
ACT 213
CCM 17715✔
CUF 714
NLD 1638
2. LUSHOTO-TANGA
ACT 375
CCM 19775✔
CDM 4402
CUF 350
3. ULANGA-MOROGORO
ACT 626
CCM 25902✔
CDM 10592
4. HANDENI MJINI-TANGA
ACT 194
CCM 12698✔
CDM 632
CUF 2522
TLP 13
5. ARUSHA MJINI-ARUSHA
ACT 359
CCM 34849
CDM 67250✔
CUF 96
Katika Majimbo haya 5 ni kwamba CCM imeshinda Majimbo 4 na CHADEMA 1.
CCM imepata jumla ya KURA 110939 na CHADEMA imepata KURA 82876 kwenye Majimbo yote 5 yaliyofanya uchaguzi ingawa katika Jimbo la Lulindi CHADEMA hawakusimamisha mgombea.
CCM ipo mbele kwa tofauti ya KURA 28663.
Majimbo ya MASASI na LUDEWA yanategemea kufanya uchaguzi wake Jumapili ya Tarehe 20 December 2015.

Epuka ajali jifunze ubora wa matairi ya gari lako

Imekuwa ni kawaida kwa watumiaji wengi kununua matairi ya magari yao bila kujali viwango vya matairi hayo ili mradi tu mtu kanunua. Kwenye Kununua matairi kuna vigezo vingi sana vinavyopelekea kuwa tairi kuwa sahihi katika mahitaji yako.

Mfano wa vitu hivyo ni Ukubwa wa tairi (size ya tairi), upana, na urefu wa tairi na uwezo wa mwisho wa spidi gari inapokimbia lakini wengi wamekuwa wakiangalia vitu vichache kama Upana, na Urefu tu bila kuangalia spidi inayotakiwa kukimbia katika matairi hayo kwa kingereza uitwa Tyre Speed rating ambapo matairi yote huwa yana ukomo wa spidi endapo gari inatembea.

Leo sasa tutakuangalizia jinsi ya kuweza kutambua spidi ya mwisho unayotakiwa kukimbia kutokana na matairi ya gari yako. Jinsi ya kutambua unachotakiwa kufanya ni kuangalia kwenye tairi yako kuna sehemu imeandikwa kwa mfano huu "255/65/R16 91W" Maana ya tarakimu hizo ni 255 ni upana wa tairi, 65 ni urefu wa tairi kutoka kwenye rim, R16 ni saizi ya rim na hiyo 91W ndio tairi speed rating yenyewe. Kwa mfano huo juu gari lenye tairi hilo spidi rating yake ni W ambayo unatakiwa kutembea spidi ya mwisho ni 168 Miles/hour au 270Km/hour.

Na hii ndio chati ya Speed rating ya tairi zote unachotakiwa kuangalia ni Herufi