Breaking News

Jumamosi, 2 Januari 2016

Soma habari za muigizaji wa filamu ya Yesu

Brian Deacon akiigiza kama Yesu ndani ya filamu ya JESUS.


Ikiwa leo ni Ijumaa kuu,siku ambayo wakristo ulimwenguni wanakumbuka mateso ya mkombozi wa ulimwengu Yesu Kristo aliyekuja duniani takribani miaka 2000 iliyopita.Gospel kitaa imeamua basi kuwaletea historia ya mtu ambaye ameigiza filamu ya Yesu inayofahamika kwa jina la ''JESUS'' ambayo iliigizwa mnamo mwaka 1979 huko nchini Israel.

GK imeamua kufanya hivi baada ya kuona ni kwa jinsi gani filamu hiyo imekuwa ikigusa maisha ya watu wengi kiasi kwamba baadhi ya watu wanasahau kwamba mtu aliyemo kwenye filamu hiyo ni mwigizaji tu na siyo Yesu.hata yeye amekiri kwamba wakati wa uigizaji alikuwa akisuluhisha mambo yaliyokuwa yakijitokeza yeye na waigizaji wenzake baada ya wao kusahau kwamba yeye si Yesu bali anaigiza tu. KARIBU.
Brian Deacon ndani ya filamu ya ''JESUS''
Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.


Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.

Brian Deacon miaka iliyofuatia baada ya kuigiza kama Yesu.

Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani.

watu wakiangalia filamu ya Yesu ambayo bwana Brian Deacon ni mwigizaji mkuu.

Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani  amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.


Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12 wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba yeye (Brian) azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni Brian Deacon, akaamua kuzungumza nao, baada ya masaa 36 walikubali kurudi kuendelea na kazi.

Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha moto,lakini anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema usiku.
watumishi wa Mungu wakiwa njiani kwenda kuonyesha filamu ya Yesu katika uinjilisti huko Kongo.
Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo lakini jibu likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio maana analeta hila zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia,baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza akaona ni kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo ya watu.


Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 133 (kwa takwimu za mwaka 2001), zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa.

Brian anawaambia watu kwamba yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza,ambapo kwa takribani miaka 20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya watu.

Kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts ya mwaka 1985, The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles.

Huyo ndiye Brian Deacon mwigizaji mkuu wa filamu ya ''JESUS''iliyoigizwa mwaka 1979 huko nchini Israel. Habari kwa msaada wa mtandao.

GOSPEL KITAA INAKUTAKIA IJUMAA KUU NJEMA YENYE BARAKA.
- See more at: http://www.gospelkitaa.co.tz/2012/04/mjue-mwigizaji-wa-filamu-ya-yesu-ambaye.html#sthash.ptWMty6L.dpuf

Kamanda Kova astaafu rasmi Jeshi la Polisi


Aliyekuwa kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova amestaafu huku akisema, katika kipindi alicholitumikia jeshi hilo, hatasahau matukio matatu maishani mwake.
Kova amestaafu baada ya kuongoza kanda hiyo tangu Juni 2008.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuwatunuku vyeti vya utumishi bora askari na raia waliotoa ushirikiano kwa polisi, kwenye viwanja vya Chuo cha Maofisa wa Polisi Kurasini, Kova ambaye kabla, alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, alisema uchapakazi wake haukuanzia huko kwani kabla ya hapo alikuwa Kigoma ambako aliongoza vita ya kuzagaa kwa silaha miongoni mwa raia.
“Ingawa sipendi kukumbuka historia hii, nilifanya kazi kubwa kule ambayo ilichangia wakubwa kuona nafaa kuja kutumika kwenye jiji hili, ambalo ni kubwa kuliko yote nchini,” alisema Kova aliyestaafu rasmi baada ya kufikisha umri wa kisheria ikiwa ni pamoja na kuongezewa mkataba na mamlaka ya uteuzi.

Matukio
Katika hafla hiyo aliyotumia kutangaza kuwa anamwachia mikoba yote Simon Siro kuwa kaimu kamanda wa kanda hiyo, Kamishna Kova alitaja matukio yanayoacha kumbukumbu kichwani mwake kuwa ni: kwanza, uvamizi uliofanywa na majambazi katika Kituo cha Polisi Stakishari; pili, kuanguka na helikopta aliyokuwamo pamoja na aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal na aliyekuwa Waziri wa Ujenzi (sasa Rais), Dk John Magufuli. Tukio la tatu ni mchakato wa Uchaguzi Mkuu uliopita.
“Muda wangu umekwisha. Nimelitumikia Jeshi la Polisi kwa zaidi ya miaka 40. Haikuwa kazi rahisi kama watu wanavyodhani. Ila namshukuru Mungu kwani sikuifanya kazi pekee yangu,” alisema.
“Kabla sijaondoka nilimuuliza IGP Ernest Mangu kama nina kosa, akanijibu sina. Ndiyo maana leo (jana), nikiwa sina kinyongo, nakabidhi kijiti hiki kwa Simon Siro,” alisema Kamishna Kova huku akimshika mkono Kamanda Siro.
Alimtaka Siro kuendeleza mazuri alioyaacha ili afanye kazi zake kwa ufanisi, lakini pia alimtaka asiwe mpole kazini na asisahau kuendelea kudai masilahi ya askari zikiwamo nyumba.
Kwa upande wake, Kamanda Siro alisema: “Natoa onyo kwa vijana wanaofanya uhalifu hasa wa kutumia pikipiki. Nitakula nao sahani moja, nikishirikiana na walinzi shirikishi kwani wahalifu hawa ni wachache sana,” alisema Siro.

Kujitosa siasa
Baada ya kupata uzoefu wa kutosha zinavyoendeshwa harakati za kisiasa kuanzia mwaka 2010 na mwaka jana, Kova amesema upo uwezekano wa yeye kujitosa kwenye siasa.
“Msinishangae siku moja nitakapojiunga na chama chochote cha siasa. Nimestaafu kulitumikia jeshi na huu ni mwanzo wa mambo mengine. Masuala yangu binafsi yanaanzia hapa,” alisema. Mbali ya siasa alisema anaweza kufanya kazi nyingine yoyote. “Naweza nikaajiriwa mahali popote na nikawajibika kama inavyotakiwa,” alisema Kova ambaye awali, alikuwa anabanwa na sheria ya utumishi wa umma kujihusisha na vyama vya siasa.

Mahita
Omary Mahita, aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi enzi za utawala wa Serikali ya Awamu ya Tatu, alimpongeza Kova kwa kazi njema aliyoifanya: “Amefanya kazi nzuri. Alishirikiana vizuri na wenzake kama inavyotakiwa na hilo limemwongezea mafanikio.”

CHANZO: MWANANCHI

Dk Makongoro amponda Dk Magufuli




MAGUFULI HAKUPUNGUZA UKUBWA WA SERIKALI AMEONGEZA.
Na Dr. Milton Makongoro Mahanga
Kwa kuteua makatibu wakuu 27 kiuhalisia rais magufuli kaunda serikali yenye wizara 27 huku akituaminisha kwamba ni wizara 19. Hivyo siyo kweli kwamba kapunguza ukubwa wa serikali bali kaongeza ukubwa wa serikali.
Sina hakika kama wasaidizi wa rais wamemshauri na kumweleza kwamba wizara si ofisi ya waziri bali wizara ni ofisi ya katibu mkuu (mtendaji mkuu, afisa masuhuli). Mtendaji mkuu ndiye mwenye dhamana. Ndiyo maana hata katika ngazi ya kata, ofisi ile inaitwa Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata siyo ofisi ya Diwani.
Kwa hiyo magufuli alipounda, kwa mfano, wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi (ambazo zilikuwa wizara mbili kabla) na kuteua makatibu wakuu (maafisa masuhuli) watatu kiuhalisia hakuunganisha wizara mbili kuwa moja bali ameunda wizara tatu kutoka mbili za awali. Ameongeza ukubwa wa serikali.
Kwa hiyo anazoita wizara tano za (1) bunge, uratibu, kazi, ajira na walemavu; (2) kilimo, mifugo, na uvuvi; (3) ujenzi, uchukuzi na mawasiliano; (4) viwanda, biashara na uwekezaji; (5) Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, na akateua makatibu wakuu 13 kwenye wizara hizo 5, kiuhalisia ameunda wizara 13 hapo ambazo kabla ya hapo zilikuwa wizara 11.
Lazima ieleweke kwamba ukubwa wa serikali hautegemei sana wingi wa mawaziri bali wingi wa makatibu wakuu. Nitaeleza kwa kutoa mfano wa gharama. Ongezeko la gharama kwa kuongeza waziri mmoja ni ndogo sana kulinganisha na kuongeza katibu mkuu mmoja. Waziri anapoteuliwa tayari anakuwa ni mbunge mwenye mshahara wake wa ubunge na kinachoongezeka ni kama laki 5 tu juu ya ule mshahara wa ubunge na gharama zingine ndogo za gari n.k., na pia mishahara na gharama za katibu muhtasi, msaidizi na dereva. Lakini katibu mkuu anaingia upya na mshahara kamili na gharama zingine nyingi na wasaidizi. Aidha kwa mfano wa wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi kwenye makatibu wakuu watatu lazima kila katibu mkuu atakuwa na idara na wakurugenzi kadhaa. Kama kwa mfano kitengo cha uvuvi kilikuwa na idara moja au mbili katibu mkuu mpya wa uvuvi atataka kuongeza idara na wakurugenzi zaidi. Hizo ni gharama za ziada kwa serikali..
Kumbuka katibu mkuu awe na naibu au hapana si hoja, hoja ni kwamba atakuwa na idara kadhaa zenye wakurugenzi (wanaotakiwa kuwa wataalam wa fani za idara yao). Kwa mfano bila kujali ukubwa wa wizara, kwa mfano, ya kilimo, ufugaji na uvuvi, rais magufuli angeteua katibu mkuu mmoja (na naibu wake) halafu akateua wakurugenzi wazuri ambao ni wataalamu kila mmoja kwenye idara za kilimo, ufugaji na uvuvi. Sasa ukiwa na wakurugenzi kama hao makatibu wakuu kila kitengo wa nini? Labda rais magufuli atuambie kwamba hatateua tena wakurugenzi wa kilimo, wa mifugo na wa uvuvi, na kwamba hao makatibu wakuu wa vitengo hivyo watatosha. Lakini hili haliwezekani.
Ukiacha hayo ya msingi sasa angalia hii mpya aliyofanya rais magufuli kwenye wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji. Ameteua naibu katibu mkuu mmoja kuwa chini ya makatibu wakuu wawili! Kwa tuliosoma "chain of command" kwenye "management" tunajua kwamba kila mtumishi lazima awe na "immediate boss" mmoja tu. Sasa huyu naibu katibu mkuu bosi wake hasa atakuwa katibu mkuu wa viwanda au katibu mkuu wa biashara na uwekezaji? Na je mabosi hawa wawili wote wakimpa kazi kwa wakati mmoja ataanza na kazi ya yupi? Na je yule ambaye kazi yake itacheleweshwa (kwa sababu naibu katibu mkuu kaanza na kazi ya katibu mkuu mwingine) atajisikiaje au atachukua hatua gani katika enzi hizi za hapa kazi tu? Au itabidi makatibu wakuu hawa wawili washauriane kwanza kabla ya kumpa majukumu naibu katibu mkuu wao?
Kwa ujumla ahadi ya magufuli kwenye kampeni kwamba ataunda serikali ndogo hakuitimiza. Ameongeza ukubwa wa serikali. Rais magufuli atambue kwamba udogo wa baraza la mawaziri kamwe si udogo wa serikali.
Dr. Milton Makongoro Mahanga

Rais Dk Magufuli awapa Makatibu Wakuu rungu

 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Makatibu Wakuu pamoja na Manaibu Katibu Wakuu wakati akifungua Semina Elekezi kwa Makatibu hao Ikulu jijini Dar es Salaam leo January 2, 2015
 Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Watoa mada katika semina elekezi hiyo wakiwa ni pamoja na (toka kulia) Makatibu Wakuu Kiongozi wastaafu Balozi Dkt. Marten Lumbanga,  Balozi Charles Sanga, Katibu Mkuu Mstaafu Ofisi ya Rais - Utumishi - Mhe. George D. Yambesi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad na wengineo
 Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wakisikiliza kwa makini Hotuba ya Ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
- See more at: http://ihumi.blogspot.com/2016/01/breaking-newzz-kutoka-ikulu-ya-rais.html#sthash.CulNdKEh.dpuf

Waislamu waliogoma wafutwa kazi Marekani

Waislamu 200 wanaofanya kazi katika kiwanda kimoja cha nyama Colorado, Marekani wamefutwa kazi baada yao kugoma.
Kiwanda cha Cargill huajiri wafanyakazi zaidi ya 2,100 Colorado
Walikuwa wamegoma kulalamikia kunyimwa uhuru wa kuswali wakiwa kazini.
Wengi wao ni wahamiaji kutoka Somalia.
Msemaji wa Baraza la Uhusiano wa Wamarekani na Waislamu Jaylani Hussein anasema wafanyakazi hao katika kiwanda cha Cargill Meat Solutions walikuwa kwa muda mrefu wameruhusiwa kuswali.
Msemaji wa kiwanda hicho cha Cargill alisema kuna uhuru wa kuabudu kiwandani lakini lazima mahitaji ya kuabudu yaambatane na mahitaji ya kazi kiwandani.
Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Haki za Kibinadamu Somalia Omar Jamal, amesema mameneja wanafaa kufahamu kwamba Waislamu huhitajika kuswali mara kadha kwa siku, hili likitegemea kipindi cha mwaka.

CUF kususia sherehe za mapinduzi Zanzibar

Chama cha Wananchi kimesema hakitashiriki maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi visiwani Zanzibar kutokana na utata kuhusu matokeo ya uchaguzi.
Chama hicho kupitia taarifa kimesema maadhimisho hayo yatafanyika “Serikali ikiwa inaongozwa na viongozi ambao hawana uhalali na ridhaa ya wananchi”.
“CUF tumesisitiza mara zote kwamba hatukubaliani na uamuzi (wa kufuta matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar),” inasema taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Mshauri wa Katibu Mkuu wa CUF Mansoor Yussuf Himid.
“Tunapenda kutumia fursa hii kuwaeleza wananchi wa Zanzibar kwamba viongozi wetu hawatoshiriki katika shughuli walizopangiwa katika ratiba ya sherehe hizi.”
Siku ya Mapinduzi huadhimishwa kila mwaka tarehe 12 Januari kukumbuka tarehe 12 Januari, 1964, siku ambayo Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ilitangazwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
Serikali ya visiwani ilikuwa imetangaza ratiba ya kufanyika kwa shughuli mbali mbali zenye lengo la kuadhimisha Mapinduzi hayo kuanzia tarehe 2 Januari hadi kilele tarehe 12 Januari katika sherehe kuu Uwanja wa Amaan, mjini Zanzibar.
“Kiuataratibu, kilele cha sherehe huongozwa na Rais ambaye yupo kikatiba. Kushiriki katika sherehe hizo ni kuhalalisha kipindi cha uongozi ambacho hakipo tena kikatiba,” taarifa ya CUF imesema.
MzozoImage copyrightZanzibar Electoral Commission
Image captionMazungumzo ya kutafuta suluhu ya mzozo huo yanaendelea
“Maalim Seif Sharif Hamad na viongozi wenziwe ndani ya Chama waliokuweko Serikalini hadi tarehe 2 Novemba, 2015 hawako tayari kuhalalisha uvunjaji wa Katiba ya Zanzibar ambayo ndiyo sheria kuu ya nchi.”
Mapema wiki hii, Chama cha Mapinduzi (CCM) kiliwataka wanachama wake wajiandae kwa marudio ya uchaguzi Zanzibar, hatua hiliyoshutumiwa na CUF. Source BBC/Swahili

Arsenal, Man Utd wang’aa EPL

Arsenal wamefungua mwanya wa alama mbili kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kuandikisha ushindi dhidi ya Newcastle, Manchester United nao wakipanda kwa ushindi dhidi ya Swansea City.
Arsenal walilaza Newcastle 1-0, bao lao wakifungiwa na Laurent Koscielny kipindi cha pili, na kufikisha alama 42.
Leicester City wanaowafuata Arsenal walipoteza nafasi ya kujiimarisha baada ya kutoka sare ya 0-0 dhidi ya Bournemouth, licha ya Bournemouth kucheza mwishoni mwa mechi na wachezaji 10 baada ya Simon Francis kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea visivyo mshambuliaji Jamie Vardy.
Riyad Mahrez alishindwa kuwafungia penalti
Uwanjani Old Trafford, ni shangwe kwa meneja Louis van Gaal baada ya vijana wake kuandikisha ushindi wa 2-1, mabao yao mawili wakifungiwa na Anthony Martial na nahodha Wayne Rooney.
ArsenalImage copyrightPA
Image captionArsenal wamo alama mbili mbele ya Leicester
Kwingineko, Southampton walilazwa 1-0 ugenini Norwich City, bao hilo likifungwa baada ya kiungo wa kati wa Southampton kutoka Kenya Victor Wanyama kupewa kadi nyekundu.
Uwanjani Stadium of Light, Sunderland wamelaza Aston Villa 3-1.
Katika mechi ya awali, Liverpool walilazwa 2-0 na West Ham.
Matokeo kamili:
  • West Ham 2-0 Liverpool
  • Arsenal 1 -0 Newcastle
  • Leicester 0-0 Bournemouth
  • Man Utd 2-1 Swansea
  • Norwich 1 -0 Southampton
  • Sunderland 3-1 Aston Villa
  • West Brom 2-1 Stoke