Breaking News
Jumapili, 3 Januari 2016
Mauaji ya mhubiri Saudi Arabia yazua joto
Marekani imeeleza wasiwasi wake kuhusu hali eneo la Mashariki ya Kati baada ya Saudi Arabia kumuua mhubiri mashuhuri wa Kishia Sheikh Nimr al-Nimr.
Marekani imesema mauaji hayo huenda yakazidisha uhasama baina ya madhehebu mbalimbali eneo hilo. Idara ya mashauri ya kigeni ya Marekani imewahimiza viongozi wa eneo hilo kutia juhudi maradufu kupunguza mvutano.
Nchini Iran, waandamanaji waliokasirishwa na mauaji ya mhubiri huyo waliwasha moto majengo ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Tehran.
Sheikh Nimr alikuwa miongoni mwa watu 47 waliouawa kwa makosa yanayohusiana na ugaidi.
Aliunga mkono maandamano dhidi ya utawala wa Saudi Arabia katika mkoa wa Mashariki wenye Washia wengi mwaka 2011.
Kupitia taarifa, msemaji wa wizara ya mashauri ya kigeni ya Marekani John Kirby ametoa wito kwa serikali ya Saudi Arabia kuheshimu na kulinda haki za kibinadamu.
Aidha, ameitaka Saudi Arabia kuhakikisha kuna haki na uwazi katika uendeshaji wa kesi.
Kuuawa kwa Sheikh Nimr kulisababisha maandamano maeneo ya Washia Mashariki ya Kati, na hasa Iran na Bahrain.
Awali, serikali ya Iran, inayoongozwa na Washia, na ambayo ni mpinzani wa Saudi Arabia inayoongozwa na Wasunni katika kanda hiyo, ilishutumu vikali mauaji ya Sheikh Nimr.
Wizara ya mashauri ya kigeni ya Iran ilisema ufalme huo wa Kisunni utalipia kitendo hicho.
Aidha, ilimwita balozi wa Saudi Arabia mjini Tehran kulalamika.
Kwa upande wake, Saudi Arabia ililalamikia balozi wa Iran kile ilichosema ni uingiliaji kati wa Tehran katika masuala ya ndani ya Riyadh.
Ebu tujikumbushe maneno ya Marehemu Mchungaji Mtikila
Simbaya tukijikumbusha, je aliyosema Marehem Mchungaji Christopher Mtikila dhidi ya Rais Dk Magufuli yameanza kuonekana?
Rwandan Pastor Sentenced To Life Imprisonment For Genocide Crimes (Photo)
A Rwandan pastor accused of leading and coordinating attacks on minority Tutsis during Rwanda’s 1994 genocide has been jailed for life, Rwanda’s high court said on Wednesday, December 30 2015.
An estimated 800,000 ethnic Tutsis and moderate Hutus were killed by dominant Hutu forces in the genocide in 100 days.
An estimated 800,000 ethnic Tutsis and moderate Hutus were killed by dominant Hutu forces in the genocide in 100 days.
Jumamosi, 2 Januari 2016
Toa maoni yako,Barabara za juu (Flyover roads)
Barabara za juu (Flyover roads) zinaanza kujengwa na Mjapan. Wanakisima unachukuliaje ukamilikaji wa Daraja la kigamboni ambalo Litaanz kutumika Februaly na uanzaji wa ujengwaji wa barabara hizi?
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)